Tangazo

December 30, 2015

VIONGOZI WAPYA WA TAHLISO WAAPISHWA RASMI,WAUNGANA NA KASI YA MAGUFULI

Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akila kiapo kulitumikia shirikisho hilo mbele ya mwanasheria HAMZA JABIRI leo Jijini Dar es salaam kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania
 Na Exaud Mtei (msaka habari) wa Habari24 blog

Uongozi mpya wa shirikisho la elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania TAHLISO umesema kuwa upo tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kasi aliyoanza nayo na kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania hasa elimu ya vyuo vikuu inakuwa ya ubora unaofaa na inaheshimika nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti  mpya wa TAHLISO  Ndugu JUMA ALLY OMARI akila kiapo leo jijini Dar es salaam
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kuwasimika viongozi wa shirikisho hilo wapya mwenyekiti mpya wa TAHLISO Tanzania Bw STANSLAUS PETER amesema kuwa kwa miaka mingi elimu ya juu nchini Tanzania imekuwa haina ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na mitaala mibovu,ukosefu wa mokopo kwa wanafunzi wengi jambo linalowakatisha tamaa wengi kusoma,ambapo amesema uongozi wake umeona kasi nzuri ya serikali ya awamu ya tano na wapo tayari kushirikiana na serikali kutatua changamoto za wanafunzi nchini.
Naibu katibu mkuu wa TAHLISO KHAMIS ELLY akiapa leo Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti huyo amesema kuwa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka huu umeonyesha kuwa serikali ya Magufuli inawajali wanafunzi kwani asilimia kubwa ya wanafunzi walipata mikopo na wengine wanaendelea kupata mikopo huku akiwataka wanafunzi kutulia kwani neema kwao inakuja kutokana na kasi ya uongozi huo mpya pamoja na ule wa serikali ya awamu ya tano.
Katibu mkuu Mtendaji mpya wa Shirikisho hilo SAGOLE WAMBURA akiapa leo

Viongozi wa TAHLISO wameapishwa leo rasmi Jijini Dar es salaam baada ya uchaguzi wa Kidemocrasia uliofanyika tarehe 23 mwezi huu na wataiongoza Taasisi hiyo kwa mwaka mmoja kwa mujibu wa katiba yao.

JOSEPH SHABAN ambaye ni muazini mpya wa shirikisho hilo Akiapa leo

Omary Idd  Naibu muazini akiapa leo tayari kulitumikia shirikisho hilo

Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa rasmi kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini

Wanahabari waliokuwa katika hafla hiyo

Picha za pamoja baada ya kula kiapo kwa viongozi hao wapya wa TAHLISO leo Jijini Dar es salaam

2015-12-29 4:29 GMT-08:00 othman maulid :
 Mshambuliaji wa timu ya Mafunzo akijiandaa kupiga mpira huku beki wa timu ya KMKM akiwa tayari kumzuiya wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1.
 Beki wa Timu ya Mafunzo akiondoa mpira golini kwao, 
 Mshambuliajhi wa Timu ya KMKM na Beki wa Timu ya Mafunzo wakiwania mpira.
Kipa wa timu ya Mafunzo akiokoa mpira ikiwa moja ya shgambulio golini kwake.
Mshamuliaji wa Timu ya KMKM akimiliki mpira huku beki wa Timu ya Mafunzo akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zabnzibar uliofanyika uwanja wa amaan timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
Beki wa timu ya Mafunzo akiondoa mpira golinin kwao, huku mshambuliaji wa timu ya KMKM akiwa tayari kuleta madhara. 
Mshambuliaji wa Timu ya KMKM akipiga mpira golini kwa timu ya Mafunzo. 
Kocha wa Timu ya Mafunzo Hemedi Moroko akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wao na  Timu ya KMKM uliofanyika uwanja wa Amaan Timu hizo zimetoka sare ya bao 
1--1
Mchezaji wa Timu ya Mafunzo na KMKM wakiwania mpira.
Kipa wa Timu ya KMKM akidaka mpira wakati wa mchezo wao na timu ya Mafunzo uliofanyika uwanja wa Amaan timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
Mshambuliaji wa timu ya Mafunzo akijiandaa kumpita beki wa timu ya KMKM wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Timu hizo zimetoka 
sare ya bao 1--1
Mchezaji wa Timu ya KMKM na Mafunzo wakiwania mpira.



Kocha Mkuu wa Timu ya KMKM Ali Bushiri (Bush) akiwakaripia wachezaji wake wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1.
Beki wa timu ya KMKM akimkata mtama mshambuliaji wa timu ya Mafunzo wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
Mchezaji wa Timu ya Mafunzo na Kmkm wakishindana nguvu wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com 

No comments: