Kijana Diana Mosha (kushoto), akifafanua jambo baada ya
kukabidhiwa msaada wa vifaa mbali mbali vya kutengenezea keki kupitia mpango wa
Airtel ‘FURSA Tunakuwezesha’, kwa meneja masoko kanda ya Dar Es Salaam James
Moillo (pili kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao Ilala, Dar
Es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni meneja masoko wa Airtel kanda ya Mbagala,
Saleh Safi akifuatiwa na meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa
Bayumi.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
Kufuatia uzinduzi wa hivi karibuni wa
Airtel FURSA msimu wa mbili, Airtel inaendelea kugusa maisha ya vijana nchini
Tanzania na kuwawezesha kufikia matarajio yao ya ujasiriamali. Leo Airtel FURSA
imemfikia kijana Diana Moshi, mwenye umri wa miaka 22 anayejihusisha na
upikaji wa keki jijini Dar Es Salaam.
Diana amepokea ruzuku katika mfumo wa
vifaa vya kufanyia kazi vikiwemo trei za keki, mashine za kuchanganyia unga wa
keki, mashine za kupambia keki, jokofu na jiko la gesi .Mbali na vifaa hivyo
Diana atapokea mafunzo maalum ya ujasiriamali na ushauri wa biashara ya keki
kutoka kwa mtaalam maalum na maarufu wa biashara ya keki hapa jijini.
Kutoka alipoanzia akiwa na mtaji mdogo sana wa kuanzia biashara,
Diana aliendelea kuwa makini na kutilia mkazo wa ndoto yake. Pamoja na ukosefu
wa vifaa Diana hakukata tamaa bali alijifunza kupitia kwa jirani na kukodisha
vifaa vya kufanyia kazi kutoka kwa wafanyabiashara wengine.
Akiwa na furaha
kubwa alisema; "Niliona Airtel FURSA kama fursa ambayo inaweza kusaidia
kupunguza mapambano na kuongeza matumaini yainua biashara yangu, ninashukuru
kwamba leo Airtel FURSA imenifikia na kuweza kubadilisha maisha yangu.
Nimeanza nikiwa na mtaji mdogo sana lakini leo Airtel imenidhihirishia kwamba
kufanya kazi kwa bidii na uvumilivu inaweza kutimiza ndoto yako ".
Diana aliahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa vile yeye sasa
anauwezo kwa kuwa na zana madhubuti za kuzalisha zaidi. "Ninaamini katika
kipindi cha muda mfupi nitaweza kuzalisha zaidi na kuajiri wengine ili kusaidia
biashara yangu. Mimi ni shuhuda wa kweli kabisa wa walengwa wa Airtel FURSA
walioomba na kupata msaada.
Ninaahadi kusaidia jamii yangu inayonizunguka
kwa sababu ninaelewa fika ni jinsi gani vijana wenzangu wanavyopata tabu huko
mtaani na sitaacha kuendelea kuwahamasisha. "
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma
kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alimpongeza Diana kwa kufwata ndoto zake na kuhimiza
vijana wengine kuiga mfano wa Diana.
Akizungumza katika hafla hiyo ya
makabidhiano Bi Bayumi alisema "Diana ametutia nguvu na kuweza
kushiriki sehemu ya safari ya ndoto zake kwani ameanza akiwa hana kitu , si kwa
mtaji tu lakini hata uzoefu wa kufanya biashara hii. Lakini leo hii ameweza
kuuza keki kupitia mitandao na kujipatia hela.
Tunaamini vifaa tunavyompatia Diana leo
vitabadilisha maisha yake na kuinua biashara yake na kuongeza wateja wengi
zaidi.
Tunawahimiza vijana wengi hapa nchini
kuchangamkia Airtel FURSA si tu inayotolewa kwa vitendea kazi bali na elimu ya
biashara ambayo imekuwa ikitolewa nchi nzima hapa Tanzania, pia kwa
kupata maelekezo ya biashara kupitia mitandao yetu ya kijamii inayosadia
kuelekeza vijana jinsi ya kukuza biashara zao, kujenga fursa kwa ajili ya
wengine na kuwa na huduma na jami zao zinazowazunguka.
Airtel, kwa mara nyingine tena katika
mpango wake wa Airtel FURSA umeahidi kuendelea kugusa maisha ya wa
Tanzania kwa kuwawezesha vijana kupitia Airtel FURSA. Hadi sasa Airtel imeweza
kufikia vijana zaidi ya 2,500 nchini Tanzania na na imeahidi
kufikia vijana zaidi ya 1500 katika kipindi cha miezi sita ijayo.
No comments:
Post a Comment