Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Prosper Mbena akimshukuru Mkurugenzi wa tigo kanda ya pwani Goodluck Charles baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 400 yaliyotolewa na kampuni ya Tigo Tanzania kwa shule 10 za jimbo la morogoro kusini. |
Mkurugenzi wa tigo kanda ya pwani Goodluck Charles akimkabidhi Afisa wa Elimu wilaya ya Morogoro vijijini Donald Pambe msaada wa madawati 400 katika shule 10 za wilaya hiyo hafla iliyofanyika katika shule ya msingi Kibangile
Februari 11 2016 Morogoro: Kampuni ya Tigo
Tanzania imetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 60
kwenye shule 10 za msingi katika mkoa wa Morogoro ikiwa ni mchango wa kampuni
hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule
za msingi nchini.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika
katika Shule ya Msingi Kibangile iliyopo Kitemu katika kata ya Matambo,
Morogoro Kusini, Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Pwani Goodluck Charles mchango huo
ni sehemu ya utekelzaji dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono shughuli
mbalimbali za maendeleo nchini.
“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa
na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini
kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa
baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi
na wengineo, "alisema Charles.
Charles alisema mwaka jana Tigo
ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya
Shinyanga, Mbeya na Iringa na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa
madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.
Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dr Rajabu Rutengwe ambaye alisema madawati hayo 400 yataboresha
mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Mporogoro na kutoa wito kwa
wadahu wengine kuunga mkono zoezi hilo.
“Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu
katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa
madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Morogoro. Ni Dhahiri
kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata
sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora Zaidi,”
alisema Dr Rutengwe.
|
No comments:
Post a Comment