Tangazo

March 24, 2016

DK. SHEIN AAPISHWA KUWA RAIS WA ZANZIBAR

Rais Mteule wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Makungu (kulia), katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja jana. PICHA: JOHN BADI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhiwa Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Makungu (kulia), baada ya kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja jana. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride maaulum la vikosi vya SMZ, baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Makungu (hayupo pichani), katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja jana. 
Sehemu ya Wananchi wakiwa wenye furaha wakati wa sherehe za kuapishwa na kukabidhiwa madaraka Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja jana. 

No comments: