Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii TAnzania (SHIWATA) umetoa salamu za rambirambi kwa familia, wanamuziki wa dansi, wadau wa muziki wa dansi nchini na wengine walioguswa na msiba wa mkongwe wa muziki nchini marehemu Mzee Kassim Mapili (Pichani) aliyefariki na kuzikwa wiki iliyopita makaburi ya Kisutu, Dar es SAlaam.
Mwenyekiti wa SHIWATA, CassimTaalib alisema marehemu Mapili atakumbukwa kwa ushirikiano, uwazi na uchangamfu kwa wanamuziki katika kipindi chote cha maisha yake.
Alisema SHIWATA imesikitishwa kuondokewa na mshauri wa wanamuziki ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi wa mtandao huo akiwakilisha Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) na muda wote wa uhai wake marehemu Mapili alikuwa akichangia ukuaji wa muziki wa dansi na kuimarika kwake ingawa umekuwa ukikabiliwa na ujio wa muziki wa kizazi kipya.
Alisema SHIWATA itamkumbuka marehemu MApili kwa uhamasishaji wake kuwartaka wasanii wajiunge na mtandao huo na kwa mara ya mwisho aliwahasisha wasanii wa fani mbalimbali kujiunga na PPF katika mkutano ulioandaliwa na mtandao huo kuwaunganisha wasanii kupata bima ya aAfya.
Marehemu Mapili ambaye alistaafu muziki katika bendi ya Polisi Jazz mwaka 1981 alikuwa mwanamuziki mwalikwa katika bendi mbalimbali.Atakumbukwa kwa wimbo wake maarufu wa Napenda nipate lau nafasi niseme nawe kidogo... alioutunga na kuimba akiwa na Bendi ya Kilwa Jazz.
Mungu ilaze roho ya marehemu mahali Pema Peponi. Amen.
No comments:
Post a Comment