Tangazo

March 22, 2016

STARTIMES YAKABIDHI MINI PADS 180 KWA WAZIRI NAPE NNAUYE KURAHISISHA UTAFITI WIZARANI

 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (wa pili kulia) akipokea moja ya Mini Pads 180 kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (wa kwanza kushoto), Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Wakishuhudia tukio hilo wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel  (kulia).
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akifurahia kupokea Mini Pads 180 kutoka kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa, Elisante Ole Gabriel na wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing na muwakilishi kutoka ubalozini Bw. Mr Gao Wei.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto), akiteta jambo baada ya kupokea Mini Pads 180 kutoka kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Pamoja naye kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dr. Lu Youqing.


Na Dotto Mwaibale

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye amepokea Mini Pads za kisasa 180 zenye thamani takribani milioni 90 kutoka kwa kampuni StarTimes Tanzania kwa ajili ya kuwarahisishia kazi wafanyakazi wa wizara yake.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo ndani ya jingo la Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mikocheni jijini Dar es Salaam, Mh. Nnauye amebainisha kuwa Mini Pads hizo zitarahisisha kwa kiasi kikubwa wafanyakazi wa wizara yake kuendana na kasi ya ukuaji wa TEHAMA katika kufanya shughuli zao hususani tafiti.

“Wizara yetu inashughulika na Sekta Nne Kubwa. Nazo ni; Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Sekta hizi ndizo zinazokamilisha jina la Wizara yetu. Wizara yangu inashirikiana na Wizara, Taasisi na wadau mbalimbali katika kuletea maendeleo wahusika katika sekta tajwa. Katika Nchi yetu tunazo Halmashauri zaidi ya 170 ambazo kimsingi kila Halmashauri inapaswa kuwa na Ofisa mmoja kwenye kila sekta zetu, hivyo maafisa 4 kwa ajili ya sekta Nne. 

Kimuundo tunakuwa na Afisa mmoja wa kila sekta kwenye kila Mkoa hivyo maafisa 4 kwenye kila Mkoa wa ngazi ya Mkoa.” Alisema Mh. Nnauye

“Baada ya kutafakari kwa kina, tukaona tuanze na kuboresha mawasiliano kwa maafisa wetu ndani ya Wizara, Baadhi ya Mikoa na pia Halmashauri. Tunaamini kwamba mawasiliano madhubuti yakiwepo, itakuwa rahisi kufanya ufuatiliaji wa kina na kuboresha utendaji. Kwa kutambua kwamba kuna haja ya kushirikisha wadau mbali mbali tuliwasiliana pia na kampuni ya Star Times ambayo ni mbia wa TBC kwa ajili ya kutusaidia wanaloweza kwa ajili ya kuanza uboreshaji wa vitendea kazi vya mawasiliano katika sekta zetu.” Aliongezea

“Ni faraja kubwa kuona kwamba wenzetu wa Sar Times wametuelewa haraka na kukubali kutusaidia vifaa hivi vya mawasiliano (Mini Pads) zipatazo 180. Kwa hakika vitatusaidia sana kuboresha utendaji kimawasiliano kwa maafisa wetu wa Wizara na pia Maafisa mawasiliano ambao ni wadau wa kutoa taarifa kwa umma,” alisema na kuhitimisha Mheshimiwa Nnauye, “Ifahamike kwamba kwa jinsi dunia inavyobadilika kwa kasi kubwa sana, masuala ya mawasiliano sio hiari tena bali ni lazima kuwa na mawasiliano ya kimkakati. 

Mpango wetu ni kwamba maafisa wote ambao wanafanya kazi kwneye Halmashauri zote, wapate mawasiliano japo hatua kwa hatua kwenye sekta zote Nne. Tunawashukuru sana kampuni ya Star Times kwa msaada huu mzuri wa kuanzia.”

Kwa  upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao alisema kuwa imekuwa ni fursa kubwa kwa kampuni kuweza kufanikisha watanzania wanatumia vifaa vinavyoendana na kasi ya maendeleo ya tekinolojia duniani kurahisisha kazi.

“Naweza kusema ni fursa ya kipekee kwa Mheshimiwa Waziri kutuona sisi StarTimes kuwa tungeweza kuwatatulia changamoto waliyokuwa nayo kwani zipo kampuni na taasisi nyingi ambazo zingeweza kufanya hivyo. Hili naweza kusema limechangiwa kwa kiasi kikubwa na jitihada tulizonazo katika kuwatumikia watanzania kwa kuwapatia huduma bora na nafuu za matangazo ya dijitali. 

Kwa kiasi kikubwa shughuli zetu tunazozifanya huwezi kuzitenganisha na maendeleo ya tekinolojia ya habari na mawasiliano. Ninaamini kupitia Mini Pads tulizozikadhi leo wafanyakazi wa wizara watakuwa na fursa ya kupata huduma zetu bila ya wasiwasi wowote.” Alifafanua Bw. Liao


“Idadi ya Mini Pads tulizozikabidhi hii leo ni 180 na tuna matumaini zitakuwa ni msaada mkubwa kwa wafanyakazi wa wizara kwa idadi iliyotajwa na mheshimiwa waziri. StarTimes tumejizatiti vya kutosha si tu kuwahudumia wateja wetu bali pia kusaidiana nao katika shughuli mbalimbali. Kwa sasa kampuni yetu imelenga zaidi katika kuwekeza na kukuza vipindi na chaneli za nyumbani ili kuwapa watanzania wenye vipaji kuweza kuonekana. Tunashukuru sana ushirikiano tunaoupata kutoka serikali kwani ndio mdau mkubwa katika shughuli za uendeshaji wetu ambao ni zaidi ya miaka mitano sasa tangu tuanze.” Alihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania.

No comments: