Afisa Uhusiano
na matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya mafanikio ya mafunzo ya stadi za ufundi yanayotolewa na
VETA kupitia mtandao wa simu ya mkononi wa Airtel yajulikanayo kama “VSOMO”
yaani VETA SOMO katika ofisi za makao makuu ya Airtel Tanzania zilizoko Moroco
jijini Dar es Saalam hapo jana.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel FURSA ikishirikiana na Mamlaka
ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) imeendelea kuwawezesha vijana kupata kozi
mbalimbali zinazotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia application
ijulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO.
Akiongea na
waandishi habari afisa Uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki alisema, “vijana
wameufurahia sana mpango huu unaowawezesha kusoma masomo kutoka VETA kwa
urahisi zaidi na kuchochea kukua kwa elimu kwa vijana wengi na kuwawezesha
kupata ujuzi wa ufundi na biashara itakayoongeza ufanisi wao.”
“Mafunzo kwa
njia ya mtandao ni rahisi na yatapatikana kwa wateja wa Airtel wenye simu
zenye mfumo wa android. Mteja atatakiwa kupakua application ya VSOMO
kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kujiandikisha
bure. Mara baada ya kumaliza masomo yake kwa 40% mwanafunzi atatakiwa
kwenda kwenye kituo cha VETA kilichopo karibu nae na kujiandikisha kwaajili ya
mafunzo kwa vitendo ambayo yatachukua muda wa wiki 2 kumaliza ikiwa ni sawa na
masaa 60 na ndipo atakapokaa kwaajili ya mtihani na kutakiwa kufaulu kwa
60% “alisisitiza Kaniki.
Aliendelea
kusema kuwa “vijana zaidi ya 19000 wamejisajili kusoma kozi mbalimbali kutoka
VETA kupitia simu zao za mkononi. Kwasasa masomo yanayopatikana ni Ufundi
pikipiki (bodaboda), Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi wa simu za mkononi,
Ufundi Alluminium, utaalamu wa maswala ya urembo na ufundi wa kuchomelea
vyuma.”
Akibainisha
hayo Kijana Saleh Shomari anayesoma kozi ya ufundi umeme kupitia
application ya VSOMO alisema “ VSOMO imekuwa msaada kwangu maana nilikuwa
natamani kusoma kozi VETA lakini sikuwa na mda wa kufika chuo cha VETA kutokana
na mihangaiko ya biashara zangu, lakini nawashukuru Airtel na VETA kulionahili
na sasa najisomea mafunzo haya ya umeme jioni nikishafunga biashara yangu na
kuweza kufikia malendo yangu ya kupata cheti kutoka VETA.”
Dangio
alimalizia akisema” Mwanafunzi atatahiniwa na kisha kuandikishwa na kutakiwa
kulipia kiasi shilingi 120,000/= kwa kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60#
kama gharama ya mafunzo hayo. Tunatoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ya
kipekee ili kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na gharama nafuu kwani gharama
ya masomo iko chini zaidi.”
No comments:
Post a Comment