Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka Shirika la Pensheni la PPF Kanda ya Ziwa, Khatibu Mussa Khatibu (kulia), akitoa semina kuhusu Umuhimu wa wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujiunga na shirika hilo ili kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo mafao ya matibabu, kutokana na kazi zao.
Kulia ni Mohamed Nyengi ambaye pia ni Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka Shirika la Pensheni la PPF Kanda ya Ziwa, akifuatilia semina hiyo iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa ajili ya wasanii wa filamu mkoani Mwanza.
Na BMG
Na George Binagi-GB Pazzo
Mafunzo kwa wasanii wa Filamu yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini mkoani Mwanza, yamefungua milango mipya ya mafanikio katika soko la filamu mkoani Mwanza, baada ya Shirika la Pensheni la PPF kuahidi kuwajengea studio ya kisasa wasanii hao ikiwa watajiunga kwa wingi na shirika hilo.
Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa wasanii hao kujiunga na huduma za PPF, Afisa Uendeshaji na Masoko wa shirika hilo Kanda ya Ziwa, Khatibu Mussa, amesema mbali na wasanii hao kunufaika na mafao yanayotolewa na shirika hilo, pia wanaweza kunufaika zaidi kwa kujengewa studio ya kisasa kwa ajili kurekodia kazi zao ambapo ameahidi kufikisha suala hilo mbele ya uongozi kwa ajili ya utekelezaji.
Baada ya kauli hiyo, Mzee Fumbuki Lubasa ambaye ni Mkufunzi Mstaafu kutoka Chuo cha Ualimu Butimba, idara ya Fasihi kwa Kiingereza na Sanaa, alisimama na kuahidi kutoa bure kiwanja chenye thamani ya takribani shilingi Milioni 20 ili ikiwa PPF itakubali kujenga nyumba kwa ajili ya studio ya wasanii wa filamu mkoani Mwanza.
Hayo yanajiri ikiwa ni juhudi za Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, aliyewataka wasanii wa filamu mkoani Mwanza kuboresha soko la filamu kwa kuwa na studio bora na ya kisasa kwa ajili ya kurekodia kazi zao pamoja na kazi nyingine ikiwemo utengenezaji wa vipindi bora na vyenye maudhui ya mtanzania kwa ajili ya kuoneshwa kwenye runinga mbalimbali nchini.
Mohamed Nyengi ambaye pia ni Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka Shirika la Pensheni la PPF Kanda ya Ziwa, akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujiunga na mfuko wa PPF. Kulia pia ni Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka Shirika la Pensheni la PPF Kanda ya Ziwa, Khatibu Mussa Khatibu.
Mzee Fumbuki Lubasa (kulia) ambaye ni Mkufunzi Mstaafu kutoka Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza, idara ya Fasihi kwa Kiingereza na Sanaa. Pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Sanaa Asilia.
Alikuwa akizungumza wakati wa warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza ambapo ametoa kiwanja chenye thamani ya takribani shilingi Milioni 20 ili wasanii wa filamu Mwanza wajengewe studio ya kisasa ya kurekodi kazi za sanaa ikiwemo filamu.
Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, baada ya kujitokeza na kutoa kiwanja kwa ajili ya wasanii wa filamu Mwanza kujengewa studio ya kisaa ya kurekodia kazi za sanaa.
Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto) akisalimiana na Afisa Uendeshaji kutoka PPF Kanda ya Ziwa, Mohamed Nyengi, baada ya kujitokeza na kutoa kiwanja kwa ajili ya wasanii wa filamu Mwanza kujengewa studio ya kisaa ya kurekodia kazi za sanaa.
Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto) akisalimiana na Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka PPF Kanda ya Ziwa, Khatibu Mussa Khatibu, baada ya kujitokeza na kutoa kiwanja kwa ajili ya wasanii wa filamu Mwanza kujengewa studio ya kisaa ya kurekodia kazi za sanaa.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, akiwahamasisha wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujiunga katika vyama vyao na kuanza kunufaika kupitia kutokana na kazi zao.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akizungumza kwenye warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Mkufunzo kutoka Chuo Kikuu Dodoma, Idara ya Habari na Ubunifu, Deodracias Nduguru, akiwafunza wasanii wa filamu mkoani Mwanza namna bora ya kujitangaza na kutangaza kazi zao ili kujulikana zaidi.
Wasanii wa filamu akiwemo Mjumbe wa Shirikisho la Filamu Taifa kutoka mkoani Mwanza, Hussein Kimu (kulia) akiwa pamoja na Myovela Mfwaisa (kushoto).
Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, Innocent Mungy, akiwasilisha mada kuhusu namna bora ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii kwenye warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza.
Amesema wasanii hao wakiitumia vyema mitandao ya kijamii wataweza kukuza soko lao la filamu ikiwemo kutangaza kazi zao na hivyo kuongeza mauzo ya kazi zao na kujiongezea kipato kupitia matangazo mbalimbali.
Wasanii wa filamu zaidi ya 300 mkoani Mwanza wakifuatilia mafunzo kutoka kwa Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, Innocent Mungy, ambaye amewasilisha mada kuhusu namna bora ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii.
Bonyeza HAPA Kuhusu Mafunzo Hayo.
No comments:
Post a Comment