Tangazo

November 11, 2016

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA SPIKA MSTAAFU SAMWEL JOHN SITTA JIJINI DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Oktoba 11, 2016. PICHA: IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimfariji Mama Margareth Sitta, Mjane wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimpa pole binti wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimpa pole Mhe. Benjamini Sitta, mtoto wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta.

Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima  za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta.

No comments: