Tangazo

April 17, 2017

MAZISHI YA MZEE JOSEPH PHILIP MAHIGA

Waombolezaji wakiwa wamebela jeneza lenye mwili Marehemu Mzee Joseph Philip Mahiga, baada ya kuwasili nyumbani kwake Msasani Makangira, ambapo baadaye ulipumzishwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi Aprili 13 mwaka huu. Aliyeshika msalaba ni Emmanuel ambaye ni mtoto wa Marehemu. Mzee Mahiga alifariki Aprili 11 katika Hospitali ya Mkombozi alipokuwa amelazwa kwa matibabu. PICHA ZOTE: JOHN BADI
CHINI NI MTIRIRIKO WA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA MSIBA
Watoto wa Marehemu (kutoka kushoto), Georgina, Hellen, Josephine, Esther na mjukuu Tamala, wakiwa wenye majonzi baada ya mwili wa mpendwa wao kuwasili nyumbani.
Dada wa Marehemu akilia kwa uchungu huku akisaidiwa na mjukuu Nounou.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa Marehemu kaka yake, Joseph Philip Mahiga.
Jaji Mkwawa akitoa heshima za mwisho.
Mmiliki wa Blog hii, John Badi akitoa heshima za mwisho.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Joseph Philip Mahiga.


No comments: