Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es saalam ,
Habibu Bukko akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa
kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO Jabir ambayo ni ushirikiano
baina ya VETA na Kampuni ya Airtel Tanzaniam. Kushoto ni Meneja wa
Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
DAR ES SALAAM
Mamlaka ya mafunzo ya ufundi VETA leo imekabidhi vyeti vya
kuhitimu masomo ya ufundi stadi kwa vijana 8 wa mkoa wa Dar es saalam baada ya
kuhitimu masomo yao ya ufundi wa umeme wa majumbani pamoja na ufundi wa
simu mara baada ya kumaliza kusoma kupitia aplikesheni ya VSOMO na
kuhitimu katika viwango vya VETA
Akikabidhi vyeti hivyo Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es
saalam , Habibu Bukko aliishukuru Airtel kwa ushirikiano wake na VETA
kupitia Aplikesheni ya VSOMO ambapo imekuwa ikifaidisha wanafunzi walioko
mbali na vyuo vya VETA kuweza kusoma VETA wakiwa popote, vilevile alipongeza
vijana hao kwa kutumia simu zao za mkonononi vyema na kuhitimu masomo ya
ufundi
Alisema jitihada hizi za Kufanikiwa kutoa Masomo ya Ufundi
stadi kupitia Aplikesheni ya VSOMO zinaenda sambamba na mikakati iliyojiwekea
VETA na serikali kwa ujumla katika kutanua wigo ili kutoa wa elimu
ya Ufundi stadi hata kwa jamii ambayo bado haifikiwa na miundombinu ya vyuo vya
VETA mahali walipo ili nao kuwawezesha kushiriki maendeleo ya jamii.
“Hadi sasa tunao zaidi ya vijana takribani 54 waliohiti masomo
yao kupitia VSOMO na kukabithiwa vyeti vyao. “nawapongeza kwa dhati vijana
hawa kwa kuhitimu masomo yao leo. Pia tunao wanafunzi 25 wanasubiri
kupangiwa masomo ya Vitendo ili kuhitimu na kupata vyeti . Nitoe wito
kwao kujiandaa vyema kuingia kwenye mafunzo ya viyendo laikini pia kwa
watanzania hususani vijana kutumia fursa hii kujisomea masomo ya ufundi
kwa kupitia mfumo huu wa VSOMO wakiwa popote VETA itawahudumua” alisema
Bukko
Akitangaza majina ya wanafunzi hao waliohitimu mafunzo
hayo Mkuu wa chuo VETA Kipawa, Eng Lucian Luteganya VSOMO nae alibainisha kuwa,
mfumo wa kusoma mafunzo ya ufundi kupitia mtandao umekuwa na tija kubwa na
kuongeza wigo kwa VETA kupokea maombi ya kutengeneza kozi maalum kulingana na
uhitaji wa wanaotaka kusoma kwa manufaa ya jamii zao. Tunachofanya leo ni
udhihirisho thabiti kuwa inawezekana kutumia mifumo mibadala katika kutoa elimu
na kufikia malengo tuliyojiwekea, tusiwe wangumu kwenda na mabadiliko
yanayoletwa na technologia kwani kwa kufanya hivyo tutazuia fursa ya kufanya
shughuli zetu kwa ufanisi.
Napenda kuwataja wahitimu wanaomaliza leo na kutunukiwa
vyeti vya VETA ni Hamadan Salum, Elvis Mahenge Simon, Mohamed Ibrahim Mohamed,
Sunday Jabil, Avitus Paul, Ridhuwani Hamidu Muhimu, Eliud Mwaikamila na
Deogratius
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi
Beatrice Singano Mallya alisema “Airtel kupitia mradi wetu wa kusaidia jamii wa
Airtel FURSA Tunajisikia fahari kuona tunaleta mabadiliko katika jamii kwa
kupitia technoligia ya mtandao wa simu. Lengo letu ni kuiwezesha jamii
kujiinua kiuchumi na kuzifikia fursa mbalimbali zinazohitaji wao kuwa na ueledi
wa kutosha. Tunaamini VSOMO italeta mabadiliko katika sekta ya elimu na
kuchochea ongezeko na nguvukazi yenye uledi ili kukudhi mahitaji ya soko la
ajira na kujiajiri
Tunaahidi kuendelea kushirikia na VETA na taasisi mbalimbali
katika kuhakikisha tunatumia techologia ya mawasiliano katika kutatua
changamoto zao mbalimbali na kuchangia katika kuboresha maisha ya jamii
zinazotuzunguka na uchumi wan chi kwa ujumla.
Mfumo wa masomo kwa njia ya Mtandao VSOMO toka kuzinduliwa
umekuwa na mafanikio makubwa ambapo hadi sasa takwimu zinaonyesha zaidi ya
vijana 33,000 tayari wamepakua application ya VSOMO kupitia simu zao za Androad
BURE, na wengine 9500 wamejiandikisha ili kujisoma kozi mbalimbali
zikiwemo za Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya
kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari.
Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za
mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma
Ufundi wa kuchomea vyuma.
|
No comments:
Post a Comment