Tangazo

December 8, 2017

Biharamulo wafurahia ujio wa Duka Jipya la Tigo



Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza akiongea na waandishi na wakazi wa Biharamulo waliohudhuria uzinduzi wa duka la kisasa la Tigo wilayani humo.


Baadhi ya wakazi na Biharamulo wakifuatilia uzinduzi wa Duka jipya la kisasa la Tigo

Meneja Mauzo wa Tigo Biharamulo, Abraham Mchau akiongea na waandishi na wakazi wa Biharamulo waliohudhuria uzinduzi wa duka la kisasa la Tigo wilayani humo.

Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, ambaye ni Afisa Habari na Mawasiliano Biharamulo, Jonathan Rwekaza(kushoto), akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa la kampuni ya Tigo wilayani humo leo. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Tigo mkoani Kagera, Sadok Phares (katikati) na Meneja Mauzo wa Tigo Biharamulo, Abraham Mchau


Afisa Mauzo wa Duka hilo, Lucy Ernest akifafanua jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza kuhusu  bidhaa mbalimbali ndani ya duka jipya la Tigo Biharamulo. 
Afisa Mauzo wa Duka hilo, Lucy Ernest akifafanua jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza kuhusu  bidhaa mbalimbali ndani ya duka jipya la Tigo Biharamulo.

Picha ya pamoja

Biharamulo, 7 Desemba, 2017- Katika mwendelezo wa harakati za kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanapata huduma bora kwa urahisi, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imezindua duka kubwa la kisasa wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera.


Duka hilo jipya linapatikana katika Jengo la Yusuph Katri lililopo Stendi ya Mabasi ya Biharamulo, mkabala na Kituo cha Polisi na lina uwezo wa kuwahudumia wateja zaidi ya 700,000 wa Tigo wanaopatikana wilayani hapo na viunga vyake.


Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua duka hilo jipya la Tigo, Meneja Mauzo wa Tigo - Biharamulo, Abraham Mchau alisema kuwa ufunguzi wa duka hilo jipya unaendana na mpango wa upanuzi na ukuaji wa kampuni hiyo ya simu unaolenga kuongeza idadi ya vituo vya huduma kwa wateja huku ikihakikisha kuwa bidhaa na huduma zote zinapatikana kwa urahisi na wateja wake nchi nzima.


‘Tigo imejizatiti kufanya uwekezaji utakaohakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa viwango vya kimataifa ili waweze kupata suluhisho muafaka kwa mahitaji yao. Ufunguzi wa duka hili la kisasa mjini Biharamulo kunafanya idadi ya maduka yetu ya Tigo kufikia 15 katika Ukanda huu wa Ziwa, huku jumla ya maduka yetu yote ya Tigo nchini ikifikia 75,’ alisema.


‘Uzinduzi huu unaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bora, za kibunifu, zinazoendana na mahitaji yao. Tunaendelea kuwekeza katika upanuzi na uboreshaji wa mtandao wetu wa simu, ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mabadiliko na faida za ulimwengu wa kidigitali unaoongozwa na Tigo,’ Mchau alifafanua.


Kwa upande wao, wakaazi wa Biharamulo wameelezea kufurahishwa kwao na ujio wa duka hilo jipya la Tigo kwani litawapunguzia adha ya kusafiri kwa mwendo mrefu kupata ufumbuzi wa matatizo yao ya simu pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za simu katika wilaya hiyo.

No comments: