Mkaguzi wa magari Sagenti, Jackson Mafuru akikagua gari la Afisa
Masoko wa Kampuni ya Airtel Prosper Mwanda wakati wa ukaguzi katika maadhimisho
ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Dar es Salaam jana.
Xxxxxxx
DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendeleza juhudi
zake za kushirikiana na jeshi la Polisi Tanzania ambapo kwa sasa wameshirikiana
na polisi kikosi cha barabarani kuitikia wito uliotolewa na Mkuu wa Kikosi cha
Polisi Trafiki kuhahakisha kuwa magari yote yanakanguliwa na kuwekewa stika za
usalama barabarani.
Kwenye zoezi hilo ambalo limefanyika kwenye makao makuu ya Airtel
jijini Dar es Salaam, maofisa wa kukangua magari kutoka Kikosi cha barabarani
walishirikiana na Kampuni ya Airtel kwenye kukagua magari ya kampuni hiyo
pamoja na ya wafanyakazi.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Afisa
Uhusiano na Matukio Airtel Tanzania Dangio Kaniki alisema kuwa usalama wa
barabarani ni la kila mtu na ndio sababu kampuni ya Airtel imeendeleza
ushirikiano wake na Polisi Kikosi cha barabarani kwenye kutimiza wito wa
Kamishna wa Trafiki Tanzania la kuhakikisha kila chombo cha moto yakiwemo
magari ya biashara, magari binafsi, bajaj pamoja na pikipiki zinakanguliwa na
kubandikwa stika za usalama barabarani.
Kwa muda mrefu tumekuwa tukishirikiana na Polisi kikosi cha
barabarani kwenye matukio mengi. Ushirikiano huu umekuwa ni muhimu ili
kupunguza ajali. Usalama wa barabarani ni jukumu la kila mtu na ndio sababu
Airtel imekuwa mbele kuhakikisha hilo linafanyika, alisema Dangio.
Leo wakaguzi wa magari wameshiriki pamoja na wafanyakazi kukangua
magari yao. Natoa shukrani kwa jeshi la polisi kitengo cha trafiki kwani kufika
kwao hapa kumeweza kuokoa muda wa wafanyakazi wetu kwenda kufanya ukaguzi. Sisi
Airtel tutaendelea kushirikiana na Polisi kuhakikisha elimu ya usalama
barabarani linafikia kila mlengwa, aliongeza Dangio.
Dangio alitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa Airtel ya
kuitikia wito wa ukaguzi wa magari ili kutimiza wajibu wa kila mtu. ‘Natoa rai
pia kwa kile dereva ambaye kwa namna moja au nyingine anakuwa anaandikiwa faini
za barabarani. Airtel Money ni suluhisho kwani ni rahisi kutumia kwa ajili ya kulipia
gharama hizo.
No comments:
Post a Comment