Diwani wa
Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Mjini Yunussa Rashid akikata utepe kuzindua
duka la kisasa la kampuni za simu za mkononi ya Airtel Tanzania ambalo
limefunguliwa mjini Kigoma juzi kwa lengo kurahishisha wateja wa kampuni hiyo
kupata huduma kwa karibu zaidi.
XXXXXXXXXXXXX
· Zaidi ya vikundi vya wajasiriamali 100 kunufaika na
huduma ya Timiza Vikoba na Mafunzo ya Tehama
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imewahasa
vikundi vya kina mama wajasiriamali kutumia fursa wanazozitoa kupitia bidhaa na
huduma mbalimbali za kibunifu ikiwemo Timiza Vikoba ili kujiendesha kidigital
na kukuza biashara zao. Hayo yalisemwa na meneja miradi wa Airtel Bi Jane
Matinde wakati wa mkutano wa viongozi wa vikundi vya kina mama wajasiriamali
jijini Dar uliondaliwa na Star Women group.
Akitoa ufafanuzi wa kina Matinde alisema
“Timiza vikoba ni huduma inayowawezesha vikundi kuweka na kuchukua mikopo
kupitia simu zao za mkononi kwa kupitia huduma ya Airtel Money, huduma
inayotolewa na Airtel kwa kushirikiana na benki ya Maendeleo.
Timiza
Vikoba inaviwezesha vikundi vya kuanzia
watu 5 hadi 50 kujisaji na kufungua akaunti ili kufaidika na huduma
ya kutuma michango yao ya kila wiki, kuomba mikopo na kufanya marejesho ya
mikopo wakiwa nyumbani au mahali popote pale kwa usalama na urahisi zaidi masaa
24 siku saba za wiki kwa gharama nafuu”.
Matinde aliwashauri wanawake hao wajarisiamali
kutumia njia za teknologia ya kisasa katika kufanya miamala ya kifedha kwa
usalama, uhakika na urahisi zaidi kupitia huduma ya Timiza Vikoba “
huduma hii itawarahisishia sana kutuma pesa za michango na marejesho
kupitia simu, itaokoa muda wa kukutana na kuweka uwazi kwani kila mwana kikundi
anapoweka pesa fedha au kuomba mkopo kila moja anapata taarifa hapohapo
nakuridhia, nawahimiza mchangamkie fursa hii.
Pamoja na huduma ya Timiza pia tunawawezesha
kupata mafunzo ya Tehama kupitia maabara ya kompyuta ya Airtel fursa iliyopo
katika shule ya msingi Kijitonyama. Tayari tunao wajasiriamali ambao
wanaendelea kunufaika na masomo haya hivvo hii pia ni fursa kwenu kujitokeza na
kujiandikisha kwa wingi. Mafunzo haya ya Tehama yatawawezesha kutunza rekodi na
mahesabu ya biashara vizuri zaidi, kutumia aplikesheni mbalimbali
kuendesha biashara zenu kwa ufanusi na kukuza mitaji alisisitiza Matinde
Kwa upande wake Mwanzilishi wa Star Women group na
mwandaji wa mkutano huo, Bi Queen Cuthbert Sendiga aliwashukuru sana Airtel kwa kuwapatia
wakinamama hao wajasiriamali fursa kupitia huduma na bidhaa zao na kuwaomba
waendelea kushirikiana nao katika kutoa fursa hizi zitakazowainua wakina
mama kwani ndio muhimili wa familia na kichochoe kikubwa katika kukuza uchumi
wa jamii na nchi kwa ujumla. Aidha aliahidi kuwahamasisha kina mama wengi
kujiunga na masomo ya Tehama kwani uelewa bado ni Mdogo na pia kutumia
technologia ya kisasa katika kuweka na kukopa kupitia huduma ya Timiza Vikoba.
Tangu kuzinduliwa kwa huduma ya Timiza Vikoba
wachama zaidi ya 261,673 na vikundi 26,158 vimeshajiandikisha huku mikopo zaidi
ya 774 yenye thamani ya shilingi milioni 49 kutolewa kwa vikundi hivyo.
No comments:
Post a Comment