Katika kupambana na
makosa ya uhalifu wa kimtandao nchini TCRA kwa kushirikiana na kampuni ya
Kingdom Heritage ilifanya semina kwa vijana yenye lengo la kuwajengea uelewa wa
namna nzuri ya matumizi na usalama Mtandao.
Semina hiyo ilifanyika
mwishoni mwaka wiki iliyopita katika ukumbi wa Buni Hub tume ya Sayansi Jijini
Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vijana kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za
serikali na binafsi.
Mwanansheria mwandamizi
kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe alipokuwa akizungumza katika warsha hiyo
alisema kulingana na ukuaji wa miundombinu ya TEHAMA inakuwa kwa kasi na
kusababisha matokeo chanya na hasi katika jamii zetu
“Katika majira haya ya
maendeleo ya TEHAMA waharifu wanatumia mwanya huo kufanya uharifu katika mifumo
mbali mbalimbali ya Kompyuta hivyo tunatakakiwa kuwa makini kwa watumiaji wa
mitandao na wadau wa TEHAMA nchini,” alisema Dk Filikunjombe.
Alisema kama TCRA
wanazidi kusisitiza kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao tena yenye
maadili ili kupunguza uhalifu huo, Kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo
cha uhalifu wa kimtandao.
Mwanzilishi wa Jamii
Forums na muwasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo alizungumzia
fursa mbalimbali zinazopatikana katika mitandao na miundombinu ya TEHAMA kwa
kuwasihi vijana waliokuwa hapo kuwa wabunifu katika majira haya na kuja na
mifumo suluhisho itakayoweza kutumika katika jamii zetu.
“Serikali pia kupitia
wizara au mamlaka zinazohusika kusapoti juhudi za vijana wabunifu katika
TEHAMA kwa miundombinu na kanuni na taratibu rafiki ili waweze
kujifanikisha katika ubunifu wao mpaka kijipatia kipato binafsi na tafa zima
kwa ujumla.” Alisema Melo.
Mtaalamu wa masuala ya
ulinzi katika mfumo ya Kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik,
Robert Matafu alizungumzia namna ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya
kimtandao na kuwa salama mtandaoni.
“Nchi nyingi za Afrika
tunakosa uelewa wa maarifa ya kujilinda na mashambulizi ya kimtandao na
kupelekea kupata hasara sana katika taasisi au watu binafsi kutokana na
mashambulizi hayo,” alisema Matafu.
Aliongeza “Takwimu
zinaonyesha taasisi nyingi afrika na Tanzania tukiwepo hatuwekezi vya kutosha
katika mifumo ya kiulinzi na usalama mtandao,kwa kufanya hivyo tunaongeza
asilimia kubwa za kupata mashambulizi ya kimtandao katika tasisi zetu,” alisema.
Awali, Mkurugenzi wa
Kampuni ya Kingdom Heritage waandaaji wa semina hiyo Tunu Bashemela
alisema wao kwa sehemu yao wanaunga mkono juhudi za serikali kupitia TCRA
katika kupambana na makosa ya uharifu wa kimtandao kwa kutoa elimu kwa umma
hasa vijana ambao ndio rika linalotumia sana mitandao.
“Ili kujua matumizi
sahihi na salama vijana mliopo hapa lazima mtambue kuwa sheria ya makosa ya
uhalifu wa kimtandao ipo na inafanya kazi lazima tuheshimu na kutii vitu
inavyotuzuia kufanya bali tutumie mitandao kwa namna za ubunifu zenye kutuletea
fedha na kujiingizia kipato,” alisema Bashemela.
Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe |
Mwanzilishi wa Jamii Forums mmoja kati ya wawasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo |
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage ambao ndio waandaaji wa semina hiyo Tunu Bashemela |
Vijana na mbalimbali watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA walioudhulia semina hiyo wakifuatilia kwa makini |
Mtendaji Mkuu wa tzNIC Abibu Ntahigiye katika mjadala wa katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini. |
Mwanzilishi wa Jamii Forums katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini. |
No comments:
Post a Comment