Tangazo

April 26, 2018

Tigo na Tecno waungana wazindua simu janja ya 4G aina ya TECNO Camon X

Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania, Eric Mkomoya (kulia) akionesha simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa simu hiyo mpya iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya simu ya Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Simu hiyo mpya ya TECNO Camon X inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na kwenye duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00#. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). 



Meneja wa Kitengo cha Ushirikiano wa Biashara wa TECNO Tanzania, Anuj Khosla (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Biashara wa Tigo, David Umoh (wa pili kushoto), Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati), Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania, Eric Mkomoya (wa pili kulia) pamoja na Meneja Msaidizi wa Masoko wa TECNO Tanzania, William Motta  wakionesha simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa simu hiyo ya TECNO Camon X iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya simu ya Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Simu mpya ya TECNO Camon X inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na kwenye duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00#. . 

Mwandishi wa Habari, John Dande (wa pili kulia) akipokea kutoka kwa  Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Biashara wa Tigo, David Umoh (wa pili kushoto)  zawadi ya simu janja mpya aina ya TECNO Camon X aliyoshinda katika droo maalum iliyofanyika wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa simu hiyo mpya ya TECNO Camon X iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya simu ya Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Simu janja za TECNO Camon X zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na kwenye duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00#. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael na kushoto ni  Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania, Eric Mkomoya.



Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania inaungana na kampuni ya simu za mkononi ya TECNO kupanua wigo wa matumizi ya simu janja (smartphone) nchini pamoja na kuwapa wateja huduma bora zaidi za kidigitali, huku wakizundua simu mpya yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X.

TECNO Camon X imejazwa of ya 3GB intaneti bure kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo, ili kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata fursa ya kufurahia  huduma za kipekee za kidigitali zinazopatikana kupitia mtandao ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G.

‘Tigo ipo katika kilele cha mageuzi ya kidigitali na ndio mtandao wa kwanza na pekee wa simu za mkononi nchini ambapo wateja wataweza kujipatia simu janja, za kisasa zaidi, zenye uwezo wa 4G za TECNO Camon X kupitia maduka yetu yote ya Tigo. Pia wateja wetu wana fursa ya kununua simu hizi janja za TECNO Camon X kwa njia ya kulipia kwa awamu kutoka kwa duka la simu la Tigo kwa kupiga *147*00#,’ Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alibainisha.

Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania Eric Mkomoya alisema ‘Tunafurahia ushirikiano huu utakaowezesha upatikanaji wa bidhaa murwa na ofa kabambe kwa Watanzania kupitia mtandao mkubwa, wa uhakika na ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G. Hii ni hatua kubwa ya ukuaji wa soko la simu nchini itakayowezesha wateja kupata simu janja ya kisasa zaidi ya TECNO Camon X kwa wakati ule ule ambapo simu hiyo inazinduliwa kote duniani”.

Umoh aliongeza kuwa, ‘Tigo inalenga kuongeza upatikanaji na matumizi ya zimu janja za kisasa nchini, huku tukihakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma bora zaidi za intaneti kupitia mtandao wetu mpana na uhakika zaidi nchini wa Tigo 4G. Ndio maana Tigo inatoa ofa ya 3GB intaneti bure kila mwezi kwa miezi sita kwa wateja wote watakaonunua simu janja ya TECNO Camon X.’

Simu inayotumia kadi mbili ya TECNO Camon X ina kioo cha kikubwa cha inchi 6, uwezo wa 3GB RAM, memori ya 16GB, camera ya mbele yenye uwezo wa  20MegaPixel (MP) na camera ya nyuma yenye uwezo wa 16 MP pamoja na uwezo wa kutambua sura. Simu hiyo pia inakuja na garantii ya miezi 13. Vyote hivi vinaifanya simu hii kuwa bora kwa mtumiaji anayehitaji simu bora. Simu janja ya TECNO Camon X itapatikana kwa bei ya TSH 449,999/- na inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini, katika duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00# na kwenye duka la mtandao la www.jumia.co.tz/tigo-shop.

No comments: