Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika siku ya
uhuru wa vyombo vya habari nchini ambayo ilifanyika kimkoa kwenye ukumbi
wa klabu ya waandishi wa Habari Jijini Tanga kushoto ni Kamanda wa
Polisi Mkoani Tanga Edward Bukombe na kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya
Waandishi wa Habari mkoani Tanga (Tanga Presse Club) Hassan Hashim
Mkuu
wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika mkutano huo
kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga
Hassani Hashim kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Lulu George
Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Presse Club) Hassan
Hashim akizungumza katika mkutano huo kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa
wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Said kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
Thobias Mwilapwa na wa kwanza kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga
Edward Bukombe
MKUU wa Takukuru mkoani Tanga,Christopher Mariba akizungumza
katika mkutano huo
Afisa
Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga
(Tanga Uwasa) Dorrah Kilo akizungumza katika mkutano huo
Frank Mapunda kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
mkoani Tanga (Takukuru) akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga
Lulu George akizungumza kulia ni Mwenyekiti Hassan Hashim
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga Lulu
George kulia akifutilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edwaed Bukombe
WAANDISHI wa Habari Mkoani Tanga wametakiwa kuwajibika kwa kufanya kazi
kwa kufuata miongozo na maadili ikiwemo kuweka uzalendo mbele kwa ajili
ya maslahi ya nchi na jamii zinazowazunguka.
Hayo yalisemwa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
wakati akizungumza katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini
ambayo ilifanyika kimkoa kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa Habari
Jijini Tanga.
Alisema iwapo watazingatia maadili na kuweka mbele uzalendo itasaidia
kuweza kuwasaidia kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi na maendeleo
kupitia vyombo vya habari ili viweze kupata mafanikio makubwa.
“Ndugu zangu niwaambie uhuru wa habari ukitumika vyema vyombo vya habari
vina mchango mkubwa kwa mkoa na nchi katika nyanja za kijamii, kiasiasa
na kiuchumi kwa kujenga jamii yenye kiu ya kuleta maendeleo “Alisema.
“Lakini pia amani na utulivu wa jamii ni muhimu zaidi kuliko vipato
vyote ...Gharama ya kurudisha amani ikivunjika ni kubwa kwa hiyo wote
tuna wajibu wa kuilinda kwa kauli zetu, vitendo vyetu na maandishi
yetu”Alisema.
Aidha alisema vyombo vya habari vina wajibu mkubwa kwenye jamii kwa
kupasha habari zenye ukweli,kujenga na kuleta matumaini kwa jamii hivyo
ni vema kuchuja na kuepuka habari zinazoleta migongano na mifarakano
katika jamii hata kama zinavutia na kuwapa vipato vya haraka.
Hata hivyo alisema vyombo vya habari ni kiungo muhimu kati ya uongozi wa
makali popote na jamii lakini pia maagizo, makatazo,fursa na taarifa
mbalimbali zitokazo kwa viongozi huwafikia wananchi kupitia vyombo vya
habari .
(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment