Tangazo

May 4, 2018

WAZIRI MWIJAGE AKABIDHI TUZO ZA RAIS ZA VIWANDA(PMAYA)

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,  akimkabidhi Tuzo ya Mshindi wa pili wawakilishi wa Kampuni ya PLASCO Ltd, kutoka (kushoto) Unguu Sulay, Edith James na Alimiya Osman, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwanda, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo mchana. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, (wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mshirika wa Taasisi ya Kaizen Tanzania, James Alva, wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho katika hafla ya utoaji Tuzo za 13 za Rais za Viwanda, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo ya Mshindi wa jumla Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL Group, Roberto Jarrin, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwanda, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo ya Mshindi wa kwanza katika Makampuni matatu makubwa (TOP 3) Meneja wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Helene Weesie, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwanda, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Charles Kimei.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo Meneja Rasilimali watu  wa Kampuni ya Alaf Tanzania, Daphne Kakonge, wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais za Viwandani. 
Afisa Masoko wa Kampuni ya Alaf Tanzania, Theresia Mmasy, akipokea cheti cha shukrani wakati wa hafla hiyo.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Cheti cha kutambua mchango wa udhamini mwakilishi wa Kampuni ya IPP, Paul Urio, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwanda, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Cheti cha kutambua mchango wa udhamini Mwenyekiti wa Kampuni ya Montage, Nestory Mapunda, wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za 13 za Rais za Viwanda, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Na Muhidin Sufiani, Dar

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema kuwa azma ya kukua kwa uchumi unategemea sekta ya viwanda na hakuna budi kuhakikisha wanatimiza vigezo vya uchumi ili ukue kwa asilimia 12 kwa mwaka, pato la taifa lisipungue chini ya asilimia 15 na ajira kuongeza kwa asilimia 40 ya ajira zote.

Mwijage amesema hayo wakati wautoaji tuzo za Rais za Viwanda (PMAYA) kwa mwaka 2017 zilizofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuwataka Shirikisho la Viwanda (CTI) kuwa wabunifu na kuzitangaza bidhaa zao ili kuweza kuingiza mapato ya asilimia 25 ya fedha za kigeni.

Akizungumza wakati wa utoaji tuzo hizo, Mwijage amesema kuwa serikali ya awamu ya tano toka iingie madarakani imeweza kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

"Mpaka sasa toka Desemba 2015 tayari tumewahamasisha wawekezaji wa ndani na wa kujenga viwanda vipya 3,306 na tunawapongeza wawekezaji wa ndani nannje kwa kuchagua kuwekeza Tanzania na kuunga mkono serikali yetu ya kukuza uchumi wa viwanda kufikia 2025, " amesema Mwijage.

" Natambua kuwa baadhi yenu mna madai mbalimbali ya kurejeshewa malipo yenu yakiwemo ya ushuru wa forodha ya 15% ya ziafa kwenye uaguzaji wa sukari kwa ajili ya matumizi ya viwanda na malipo ya marejesho ya ongezeko la thamani," 
Mwijage amesema zipo changamoto zinazotokana na wenye viwanda wenyewe ikiwemo udhaifu wa kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi ya Tanzania unasababisha bidhaa za ndani kutokufahamika vizuti miongoni mwa watanzania na watuamiaji wa nje.

Mwijage amesema kupitia baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) itahakikisha watanzania wote wanashiriki katika ujenzi wa uchumi. Serikali kupitia baraza la uwezeshaji lina miradi ya kimkakati ya kusaidia viwanda vyetu na watanzania kwa ujumla kupata fursa mbalimbali zilizopo. 

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CTI Dkt. Samwel Nyantahe ameishukuru serikali kwa kuweka mijadala ya kuwasaidia watanzania wafanyabiashara hasa wenye viwanda  na baada ya serikali ya awamu ya tano kuja na sera ya ujenzi wa viwanda watanzania wengi wamejitokeza kuanzisha viwanda mbalimbali kwa azma ya kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda.

Aidha ameeleza kuwa katika maadhimisho ya miaka 13 katika utoaji wa tuzo mwaka 2016 mheshimiwa Rais alipendekeza kuhusisha sekta zote na wasio wanachama  wahusishwe na tuzo ya matumizi bora nishati viwandani ilianzishwa.

Mashindano hayo yataleta ushindani mkubwa katika sekta ya viwanda hali itakayopelekea kukuwa kwa uchumi  na kuongeza pato la taifa.

Katika tuzo za mwaka 2017  kampuni ya bia ya Tanzania Breweries (TBL)  iliweza kupata ushindi wa jumla katika viwanda vyote vinavyozalisha bidhaa mbalimbali wakifuatiwa na Zenufa na mshindi wa tatu ni Plasco  Ltd

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA





 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo, CEO wa Kampuni ya Jambo Plastics Ltd, Rupa Suchack.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi cheti Mshirika wa Taasisi ya Kaizen Tanzania, James Alva na msidizi wake Beatrice Kithinji, wakati wa hafla hiyo.
 Wasnii wa Kikundi cha Sanaa cha Safi Theatre wakitoa burudani

No comments: