Tangazo

September 14, 2011

CUF yazindua kampeni Igunga

"IGUNGA 'HATUTAKI VITA" mmoja wa wafuasi wa CUF (kushoto) akiwa na bango linalosomeka hivyo, wakati wa maandamano ya kumpokea Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye baadaye alizindua kampeni za chama hicho katika viwanja vya kumbukumbu ya Samora mjini Igunga mkoani Tabora.
HATUMWAGII TINDIKALI KAMA WAO" moja wa wafuasi wa CUF akiwa na bango linalosomeka hivyo, wakati wa maandamano ya kumpokea Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye baadaye alizindua kampeni za chama hicho katika viwanja vya kumbukumbu ya Samora mjini Igunga mkoani Tabora. Wiki iliyopita mfuasi mmoja wa CCM alimwagiwa tindikali na watu wanaodaiwa kuwa wa CHADEMA.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwa na mgombea Ubunge wa chama hicho Leopold Mahona kwenye mkokoteni wa punda na katika maandamano ya wanachama kwenda katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho.
Profesa Lipumba akizungumza jambo na mgombea ubunge wa chama cheke, Leopold  Mahona.
Mlianzi wa CUF (kulia) akiwa kazini wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho.

No comments: