Tangazo

September 15, 2011

MIKATABA YA UJENZI WA VIWANJA VYA NDEGE VYA BUKOBA, TABORA NA KIGOMA YATIWA SAINI LEO

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TAA), Suleiman .S. Suleiman (kushoto) pamona na Mhandisi Mwandamizi wa Kampuni ya  SINOHYDRO CORPORATION LTD Tawi la Afika Mashariki, Qin Chao wakitiliana saini mikataba ya ukarabati wa kiwanja cha ndege  cha Kigoma katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Sept.15, 2011 ikiwa katika muendelezo wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika sekta ya Uchukuzi. Waliosimama (kutoka kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omari Chambo, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Omari Nundu na Naibu wake, Athuman Mfutakamba. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TAA), Suleiman S. Suleiman akitoa taarifa  jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kusaini mikataba ya ukarabati wa viwanja vya ndege vya Bukoba, Tabora na Kigoma ikiwa ni moja ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru katika sekta ya Uchukuzi.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Sekta ya Usafiri wa Anga (TAA) wakifuatilia hafla ya utiaji saini.
Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa wizara hiyo na makandarasi mara baada ya hafla hiyo.

No comments: