Waheshimiwa wabunge wote wa Majimbo ya mkoa wa Dodoma, wakuu wa Wilaya zote na mkuu wa mkoa wa Dodoma, ni miongoni mwa wageni mashuhuri walio alikwa kuhudhuria shindano la kumpata mrembo wa utalii wa mkoa wa Dodoma 22-10-2011.
Shindano hilo limepangwa kufanyika katika ukumbi wa hoteli ya kitalii ya New Dodoma hoteli, na kushirikisha jumla ya warembo kumi na tano toka wilaya zote za mkoa wa Dodoma, ambao hivi sasa wana endelea na kambi ya mazoezi katika Hoteli hiyo ya New Dodoma Hotel chini ya mkufunzi wao Neema Isdory (Miss Utalii Njombe 2010/2011) na Tabia Msuta (Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya Kati 2010/2011.
Shindano hilo ambalo linaandaliwa na Miss Tourism Tanzania Organisation mkoa wa Dodoma, linatarajiwa kuvuta hisia za wakazi wengi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla, kutokana na ubora wa warembo waliojitokeza kuwania Taji hilo kubwa na la pekee la Utalii mkoani Dodoma na ushindani mkubwa uliopo miongoni mwa washiriki.

Pia hamasa ya kila Mbunge, mkuu wa wilaya na wananchi kutaka mrembo wa jimbo lake na wilaya yake kushinda taji hilo inachochea ushindani na mvuto zaidi wa shindano hilo na kusababisha karibu kila mkazi na mpenzi wa sanaa ya urembo mkoani humo kutaka kuhudhuria na kushudia balozi wa Utalii wa mkoa huo akipatikana hiyo tarehe 22-10-2011.
Mkurugenzi wa Miss Tourism Organisation Mkoa wa Dodoma Bwana Charles Gabriel amewataka wakazi wa Dodoma na Maeneo ya Jirani kujitokeza kwa wingi katika kushuhudia Mabinti Utalii wa mkoa huo wakionyesha na kutangaza Utamaduni, Utalii, Mitindo na mianya ya uwekezaji ya mkoa wa Dodoma, na uwezo mkubwa wa kuimba na kucheza ngoma na nyimbo za asili ya Dodoma, jukwaani na nje ya jukwaa huku wakitangaza Utalii na Utamaduni wa Majimbo na wilaya zao.
“…….Maandalizi yana endelea vizuri tunaomba wadhamini wajitokeze zaidi kusaidia shindano hili ambalo ndio pekee Alama ya Urithi wa Mkoa wa Dodoma na linalotoa fulsa kwa makampuni, wafanyabiashara na watu binafsi kujitangaza na kutangaza bidhaa zao, kimkoa, kitaifa na hata kimataifa kupitia matangazo ya ukumbini, redioni, magazetini, Televisheni ,Mabango ya Barabarani, Mitaani na katika mitandao ya Tovuti za kitaifa na kimataifa” alisema Charles Gabriel ambaye pia ni Mratibu mkuu wa shindano hilo.
Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Octoba 2011,lakini kutokana na mabadiliko ya kalenda ya mashindano yaliyo fanywa na Bodi ya Taifa ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania sasa litafanyika 22/10/2011.
Akithibitisha mabadiliko hayo ya kalenda Rais wa mashindano hayo nchini, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bara la Afrika wa Miss Utalii Dunia na Miss Umoja wa Mataifa Gideon Chipungahelo alifafanua kuwa mabadiliko hayo ya kalenda ya kitaifa ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania, pamoja na kulenga kuboresha zaidi mashindano na maandalizi ya fainali za kanda na mikoa ikiwemo kutoa muda na fulsa zaidi kwa waandaaji kpata wadhamini na wadhamini kujitokeza na kujiandaa, pia yamechangiwa pia na mabadiliko ya kalenda ya mashindano ya Dunia na kimataifa, fainali za Wilaya, Mikoa, Kanda na Kanda maalum za Vyuo Vikuu zitaanza Oktoba 7, 2011 na kukamilika mwanzoni mwa Februari 2012, huku fainali za Taifa zikifanyika kati ya Machi na Aprili 2012 katika mkoa utakao tangazwa katika uzinduzi rasmi wa kauli mbiu na msimu wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2011/2012 utakao fanyika sambamba na Fainali za Miss Utalii Dodoma 2011/2012.
Mikoa na kanda karibu zote nchini wapo katika maandalizi ya fainali za mikoa na kanda zao, ikiwemo mikoa ya na tarehe za mashindano yao katika mabano Mara (7-10-2011), Shinyanga (29-10-2011), Njombe ( 26-11-2011), Iringa (28-10-2011), Kanda ya Kusini ( 2-12-2011), Kanda ya Kaskazini ( 3-12-2011), Dodoma ( 22-10-2011),Vyuo Vikuu Kanda ya Kati (8-12-2011),Kanda ya Magharibi (11-12-2011), Kanda ya Mashariki (4-2-2012),Dar Es Salaam (28-1-2012), Kinondoni (9-12-2011),Temeke (31-12-2012),Ilala (24-12-2011),Pwani (25-12-2011), Kanda ya Ziwa (26-11-2011), Vyuo Vikuu Kanda ya Magharibi (21-1-2012),Morogoro (24-12-2011),Tabora (29-10-2011), aidha kalenda na tarehe kwa fainali za mikoa yote na kanda zote itatangazwa rasmi 5-10-2011 katika mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa jijini Dar es Salaam.
Fainali za mwaka huu katika ngazi zote zinalenga, kuhamasisha na kutilia mkazo zaidi katika kuhamasisha Utamaduni, Utalii wa Ndani, Utalii wa Kitamaduni, Uzalendo kwa taifa na utumiaji wa Bidhaa za Tanzania, vita dhidi ya uharibifu wa Mazingira, Uvuvi haramu, Uwindaji Haramu ,.Mila Kongwe, Mila Potofu, na vita dhidi ya Ujinga, Umasikini na Maradhi kupitia Utalii.
Wadhamini waliojitokeza ni pamoja na Asante Water, Kifimbo Radio, New Dodoma Hotel, Ngoto Funiture, Royal Vilage, Clouds Fm Radio, TANAPA, Ngorongoro Creater, VETA Hotel, Side Way Lodge, Shabibi Buss Service, Moronga By Makai Enterprises, Tanzania Daima & Sayari News Paper, Image Masters, Papaa Msofe, Zizzuu Fasheni, Dar City College, Kumekucha Action Mart, Viovena & Co LTD, pamoja na Waheshimiwa Wabunge wa Dodoma.

No comments:
Post a Comment