Tangazo

September 5, 2011

MISS/BINTI UTALII DODOMA SASA KUFANYIKA OKTOBA 1, 2011

Uongozi wa Miss Tourism Tanzania Organisation mkoani Dodoma, umesogeza mbele shindano la kumsaka Miss/Binti Utalii Dodoma 2011/2012 hadi 1-10-2011, badala ya tarehe 17-9-2011 iliyo kuwa imepangwa awali.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyo tolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mkoa wa Dodoma wa Miss Tourism Tanzania Organisation, Charles Aloyce Gabriel, kusogezwa mbele kwa fainali hizo za mkoa wa Dodoma kumetokana na kupisha semina elekezi ya kitaifa ya wakurugenzi ,viongozi na waandaaji wa Miss / Binti Utalii Tanzania wa Wilaya, Mikoa na Taifa, ambayo itafanyika 7-9-2011 jijini Dar Es Salaam na sherehe za uzinduzi rasmi wa mashindano ya Miss /Binti Utalii Tanzania 2011/2012 utakaofanyika 17-9-2011 mjini Dodoma.

“Viongozi wote wa ngazi za wilaya, mikoa, kanda na Taifa tutakuwa Dar es Salaam kwaajili ya semina elekezi ya kitaifa na baada ya semina hiyo elekezi tutakuwa katika maandalizi ya uzinduzi wa kitaifa wa Mashindano ya Miss Utalii/Binti Utalii Tanzania 2011/2012 ambao utafanyika mkoani kwetu Dodoma 17-9-2011, pia kwa mujibu wa utaratibu hatutaweza kufanya shindano kabla ya uzinduzi na semina elekezi ya kitaifa ambayo awali ilipangwa kufanyika mwanzoni mwa Septemba mwaka huu” alisema  Gabriel.

Shindano la Miss/Binti Utalii Dodoma lina dhaminiwa na ASANTE WATER, NEW DODOMA HOTEL,ROYAL VILLAGE HOTEL,SHABIBY BUS SERVICES,KIFIMBO FM RADIO na SIDE WAY LODGE za Dodoma ,wengine ni MAMLAKA YA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) NA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO (NCAA),CLOUDS FM RADIO,IMAGE MASTERS,AUCLAND TOURS & SAFARIES na PAPA MSOFE za Dar es Salaam.

Tunaomba makampuni, mashirika na watu binafsi wajitokeze kudhamini shindano hili, ambalo linalenga kutangaza Utalii, Utamaduni na Mianya ya uwekezaji ya mkoa wa Dodoma kitaifa na kimataifa, pia kuhamasisha Utalii wa Ndani, Utalii wa Kitamaduni, vita dhidi ya uharibifu wa Mazingira, Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Maradhi, Ujinga, Umasikini ,Tamaduni Kongwe na Potofu.

Jumla ya mabinti 18 wata shindano kuwania taji hilo la ubalozi wa utalii wa mkoa wa Dodoma 2011/2012, ambapo si chini ya washindi watano wa kwanza watawakilisha mkoa wa Dodoma katika mashindano ya kanda ya Magharibi ya Miss /Binti Utalii Tanzania 2011/2012 yatakayo fanyika mwezi Disemba 2011 mkoani Tabora na kushirikisha washindi wa mikoa ya Singida, Tabora, Dodoma, Kigoma na Katavi.

Tayari zaidi ya warembo 12 wamesha chukua na kurudisha fomu za kuomba kushiriki mashindano hayo makubwa kufanyika mkoani Dodoma. Walio chukua na kurudisha fomu hizo ni pamoja na Diana Mulokozi, Martha Simon yohana, Magreth William Kapelle, Taus Shaaban Ally, Axer Sostenes Petre, Bahati Mwinyi Masanja, Sekilonge Evarist Mgongolwa, Joyce Thomas Mwakibinga, Khadija Ally Abubakari, Jacline John Leshange, Neema Evaristo, Tabia Kalange na Joyce Shendago. Fomu zina endelea kutolewa kwa wanao taka kushiriki , zina patikana Dodoma Hotel, VETA Hotel, Asante Water, Side Way Lodge na Kifimbo FM ,mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni 10-9-2011,siku ambayo pia kambi ya mazoezi itaanza katika hoteli ya New Dodoma Hotel.

No comments: