Tangazo

September 5, 2011

SEMINA ELEKEZI MISS UTALII TANZANIA KUFANYIKA SEPTEMBA 7, 2011

Gideon E.G. Chipungahelo –Rais Miss Tourism
Tanzania Organisation
Bodi ya wakurugenzi ya Miss Tourism Tanzania Organisation, kampuni yenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imeandaa semina elekezi kwa viongozi na waandaaji wa mashindano hayo wa ngazi zote za Wilaya, Mikoa, Kanda na Taifa itakayo fanyika 7-9-2011 katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuanzia saa tatu Asubuhi, Semina hiyo pia itahudhuriwa na wana habari na vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Malengo ya semina hiyo imeandaliwa kwa lengo la kuwaelimisha viongozi na waandaaji wa ngazi zote wajibu na majukumu yao, baada ya kuwa wameteuliwa hivi karibuni kushika nyadhifa mbalimbali baada ya mabadiliko ya mfumo wa uongozi na mashindano ya Miss Utalii Tanzania yaliyo fanyika mapema mwaka huu, baada ya kikao cha tathmini ya mashindano hayo baina ya waandaaji wa Taifa, BASATA na wadau mbalimbali wa sanaa,utalii na utaduni.

Katika semina hiyo, washiriki wataelimishwa, mfumo kanuni na taratibu za mashindano ya Miss Utalii Tanzania, ambao ni tofauti sana na mashindano mengine ya urembo, kwani unalenga na kujikita zaidi katika kutangaza utalii, utamaduni na mianya ya uwekezaji. Pia kuhamasisha utalii wa ndani, utalii wa kitamaduni, vita dhidi ya uharibifu wa mazingira, uwindaji haramu, uvuvi haramu, umasikini, Maradhi, Ujinga, Tamaduni kongwe na potofu. Kutakuwa na watoa mada mbalimbali kuhusiana na Malengo hayo yote ya mashindano haya kutoka taasisi mbalimbali za Utalii, Utamaduni, Mazingira, Elimu, Afya, Habari na Sanaa wakiwemo wa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Wakurugenzi watakao hudhuria seminan hiyo ni pamoja na Charles Aloyce Gabriel ( Dodoma/Vyuo Vikuu Kanda ya Kati), Sophia Dio (Wilaya ya Kinondoni), Mwasiti Gange ( Kanda ya Kusini), Francis N Mhando ( Vyuo Vikuu Kanda ya Kusini),peter M. Kaiza (Vyuo Vikuu Kanda ya Magharibi),Clemence Kambengwa ( Kanda ya Mashariki),Dimo Debwe na Emanuel Manase (Manyara), Bertha F. Mbiro (Ruvuma), Mukhsin Mambo ( Mara, Simiu, Geita na Kanda ya Ziwa),Majid Mohamed (Arusha), Edwin James Ngere  na Brian Bryson Kikoti (Kilimanjaro), Juma Mwege na Neema Mallango (Kanda ya Kaskazini),Frank Kananura ( Kanda ya Kati),Amina Haruna (Kigoma).

Wengine ni pamoja na Anna Peter (Dar es Salaam), Dennis Mponji ( Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini), John Kalonga ( Kagera na Vyuo Vikuu Kanda ya Mashariki), Adam Bernad (Singida na Shinyanga), Francis Samwel (Tanga na Mtwara),Boniface Peter ( Lindi), Kasim Mpenda (Morogoro), Daisy Vedasto (Temeke),Mack Denis (Rukwa),Linda Masanche (Pwani),Richard Buhembo  (Katavi),Faraja Samwel (Njombe),Diana Henry (Ilala),Silvia Mwamnyange (Mbeya),Sharon Athumani (Iringa).

Wakurugenzi wa kamati ya Taifa ni pamoja na Grass Kihongozi, Idrissa Mzilai, Abdalla Uweje Kumekucha, Violet Kaberege, Joachim Nkwabi, Pendaeli Omari, Clifford Mario Ndimbo, Rehema Salim, Godwin Gondwe, Baruani Mhuza, Fred Mwanjala, Clemence Kambengwa, John Kalonga na Francis Samwel Chipungahelo.

Bodi inaamini kuwa baada ya semina hiyo, viongozi na waandaaji wa ngazi zote watakuwa wameiva kwa ajili ya kufanya mapinduzi makubwa ya ubora na hadhi ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania, hivyo kuwa na warembo wenye kufikia viwango vya kimataifa kuanzia ngazi za chini, ili wakishinda wawe warembo wa kiwango cha juu kabisa kuwakilisha vyema kanda zao na mikoa yao katika fainali za Taifa zilizo pangwa kufanyika Mwezi Februari 2012, baada ya kukamilika kwa fainali za mikoa na kanda ambazo zitaanza rasmi Mwezi Octoba 2011 na kukamilika Mwezi Januari 2012.
Imetolewa na:
Gideon E.G. Chipungahelo –Rais Miss Tourism
Tanzania Organisation

No comments: