Tangazo

September 5, 2011

VODACOM MISS TANZANIA 2011 KUIBUKA NA GARI AINA YA JEEP MPYA LENYE THAMANI YA MILIONI 72/-

Warembo watakaoshindania taji la Vodacom Miss Tanzania wakiwa wamelizunguka gari kwa picha ya pamoja.
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Alfred Minja (kushoto) na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania, George Rwehumbiza wakilifunua gari aina ya JEEP ambalo limetolewa kama zawadi ya Vodacom Miss Tanzania 2011 lenye thamani ya milioni 72/-.  Gari hilo limetengenezwa nchini Marekani. Hafla ya kuonyesha zawadi hiyo imefanyika asubuhi hii katika duka la kampuni ya CFAO Motors lililopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia  ni Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Alfred Minja (katikati) na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza wakikabidhi funguo za gari lililotolewa na kampuni hiyo kama zawadi ya Vodacom Miss Tanzania kwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga.

No comments: