Afisa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Bi. Dangio Kaniki (kulia) akiongea kwa simu na mshindi wa promosheni ya KWANJUKA wakati wa droo ya mwisho ya promosheni hiyo iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam leo ambapo Bw. Majid Amir aliibuka mshindi wa milioni 20/-. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando pamoja na Mkaguzi ku toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Humudi Abdul Hussein. Promosheni hiyo imefikia mwisho leo ambapo washindi wengine walioibuka na milioni 1/- kila mmoja ni David Kirongora, Donald Bazilai, Kalesho Jones na walioibuka na milioni 5/- ni Said Ismail na Richard Mbikila. |
No comments:
Post a Comment