Tangazo

September 23, 2011

RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALIMBALI HUKO MAREKANI

 Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Bwana Ted Alemayhu,Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa US Doctors for Africa aliyemtembelea Rais Kikwete katika hoteli ya Jumeirah iliyoko jijini New York tarehe 22.9.2011
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na viongozi wa makampuni ya Sithe Global, iliyowakilishwa na Bwana Bruce Wrobel ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa makampuni hayo na Bwana Garrett Moran wa Blackstone Group  kuhusu uwekezaji katika Tanzania katika nyanja za Nishati na Miundombinu. Mazungumzo hayo yalifanyika katika hoteli ya Jumeirah huko New York tarehe 22.9.2011.
Rais Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Millenium Challenge Corporation Bwana Daniel Yohannes katika hoteli ya Jumeirah jijini New York mara tu baada ya Rais Kikwete kumaliza kuhutubia mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 22.9.2011. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI

No comments: