Rais, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Hajat Amina Mrisho kufuatia vifo vya watu 10 na wengine 19 kujeruhiwa kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea tarehe 14 Septemba, 2011 katika kijiji cha Mwindu wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani baada ya basi la Kampuni ya Grazia Safari’s kupinduka likitokea Songea kuelekea Dar es Salaam.
Nimeshtushwa, na kusikitishwa sana kwa Taifa letu kupoteza, kwa mara nyingine, roho za Watanzania wenzetu 10 waliofariki kutokana na ajali mbaya ya barabarani katika eneo la mkoa wako,” amesema Rais Kikwete katika
salamu zake na kuongeza,
“Naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hii mbaya. Nawahakikishia kwamba nipo pamoja na familia hizo katika kipindi chote cha maombolezo kwani msiba
huu ni wetu sote.”
Rais Kikwete amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azilaze pema peponi roho za marehemu wote. Aidha, amesema anawaombea kwa Mola wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo wapone haraka ili waweze kuungana tena na familia zao na kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Amesema kutokana na kukithiri kwa ajali za barabarani ambazo zimeendelea kulinyang’anya Taifa nguvukazi muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, vyombo vyote vinavyohusika na usalama wa barabarani havina budi kusimamia kwa karibu mwenendo wa vyombo vya usafirishaji wa abiria ili kuepusha kutokea kwa ajali zaidi za barabarani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Septemba, 2011

No comments:
Post a Comment