Tangazo

October 13, 2011

D. C. MSUYA AZUNGUMZA NA WANAHISA WA TBL

Waziri Mkuu mstaafu, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cleopa Msuya (wa pili kulia), akihutubia katika mkutano mkuu wa mwaka wa 38 wa wanahisa wa kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche na (kutoka kushoto) ni viongozi wa kampuni hiyo na Katibu wa kampuni hiyo, Haruna Ntahena.
Mwanahisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Eddy Mushi akichangia mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa 38 wa wanahisa wa kampuni hiyo, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Miradi Maalum, Phocus Lasway (kushoto), akifafanua jambo kuhusu mpango wa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo wa kilimo cha shayiri nchini. zao hilo linatumika kutengenezea bia.
Mwanahisa wa TBL, Grace Nabur akichangia hoja katika mkutano huo.
Mwanahisa wa TBL, Mzee Kibonde kutoka Rungwe mkoani Mbeya, akichangia hoja wakati wa mkutano huo.

Waziri Mkuu mstaafu, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cleopa Msuya (kulia), akiagana na wanahisa baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa mwaka wa 38 wa wanahisa wa kampuni hiyo, Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa TBL, waliofanikisha mkutano huo.

No comments: