Tangazo

October 11, 2011

Maofisa Masoko na Mauzo wa Airtel Tanzania wapata Mafunzo Maalum

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Sam Elangallor akionyesha mtaala utakaotumika kwenye mafunzo ya maafisa masoko na mauzo wa kampuni hiyo ili kujitengenezea utaalam zaidi wa kutoa  huduma bora kwa wateja wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya maofisa masoko na mauzo wa kampuni ya Airtel wa mikoa yote tanzania mafunzo hayo yanayojulikana kama 'Airtel Centum Sales University'.  
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Sam Elangallor akimkabidhi  kabrasha Meneja Mauzo wa kanda Pwani Bw Godfrey Kavishe wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya maofisa masoko na mauzo wa kampuni ya Airtel wa mikoa.
                                            ***************************************

Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi iliyoonea na inayoongooza kwa kutoa huduma  za gharama nafuu nchini. Leo imezindua mpango mpya wa kuwaongezea ujuzi wafanyakazi wake kuhakikisha wateja wa Airtel wanapata huduma bora zaidi.

 Mafunzo haya ni muongozo kwa ajili ya timu za mauzo na usambazaji, akiongea katika uzinduzi huo mkurugenzi mkuu wa Airtel bwana Sam Elangalloor alisema, “leo tunazindua rasmi Chuo cha mauzo nchini Tanzania, ambacho kimeundwa kwa mtazamo mahiri ili kutatua matatizo na kujibu maswali mengi ambayo wafanyakazi wetu wamekuwa wakikabiliana nayo katika shughuli zao za kila siku kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora kila siku.

Tunadhamini wafanyakazi wetu ambao ni rasilimali yetu kubwa kuliko zote na ndio maana tumeelekeza jitihada zetu kwenye kuongeza ujuzi na ndio maana tumeunda mafunzo haya kuongeza kiwango cha ufanisi na utoaji Huduma za hali ya juu kwa watanzania wote pande  zote za nchi hii .

 Nchini Tanzania tayari mafunzo hayo yameshaanza kwa kushirkisha jumla ya wanaofanyakazi 55 toka kitengo cha kuhudumia wateja kwa kusambaza bidhaa na Huduma kwa wateja kutoka mikoa yote.

 (Airtel Centum Sales University) ni maendeleo ndani ya “Ujuzi Mahiri”. Chuo hiki kinatilia mkazo shughuli mbalimbali hasa katika vitengo vya mauzi na usambazaji kuhakikisha kile kilichofundishwa kinafanyiwa kazi katika shughuli za kila siku. Mafunzo haya yatachukua muda wa miaka miwili na nusu na yatakuwa na ngazi tano kuanzia uuzaji mpaka ngazi ya juu kabisa ya ushindi.

No comments: