Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Naibu Waziri wa Ujenzi Dk. Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kunduchi Beach juzi. |
Kwa mujibu wa Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa ambaye pia ni msemaji wa familia amesema hali ya ngozi Dk. Mwakyembe ni mbaya, japokuwa ana nguvu zake na fahamu na anaongea bila shida na anatembea mwenyewe. Viongozi kadhaa akiwemo Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli walikuwepo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar kumsindikiza Dk. Mwakyembe, ambaye jana alitembelewa na Rais Jakaya Kikwete nyumbani kwake Mbezi Beach.
Kwa mujibu wa mke wa Dk. Mwakyembe, Mama Linah Mwakyembe, daktari wa mumewe amesema mgonjwa anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kitaalamu kama Exfoliative Dermatitis. “Alianza kuugua muda mrefu kidogo, kama miezi mitatu iliyopita, hali hiyo ilikuwa inatokea na kupotea hadi sasa ambapo hali imekuwa mbaya zaidi,” alisema.
Alisema madaktari waliomfanyia uchunguzi kwa nyakati tofauti katika kipindi hicho walitoa majibu tofauti na kuongeza kuwa wapo waliosema hali hiyo ilisababishwa na kisukari na mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kulikuwa na chembechembe za sumu katika damu yake.
“Baada ya ngozi yake kubadilika sana na hali kuwa mbaya, tulienda hospitali na madaktari walitupa majibu tofauti, wapo waliosema ni kisukari na kuna mwingine alisema kuna chembechembe za sumu,” alisema Linah na kufafanua kuwa daktari aliyedai hivyo hakuwapa maelezo zaidi. Kwa mujibu wa Linah, ngozi ya Dk. Mwakyembe inawasha na inakuwa kama inatoa mba mwili mzima hadi kichwani.
No comments:
Post a Comment