Tangazo

October 27, 2011

Mapigano na mvua nchini Somalia 'yazidisha njaa'

Wanajeshi wa Kenya wawasaka Al Shabaab nchini Somalia
Mashambulio ya wanajeshi nchini Somalia na mvua kubwa inayonyesha imefanya juhudi za kutoa msaada kwa raia kuwa ngumu zaidi, Umoja wa Mataifa umeonya.

Watu milioni nne nchini Somalia wanahitaji msaada wa chakula kutokana na njaa na ukame.

Siku kumi na mbili zilizopita, jeshi la Kenya liliingia Somalia kushambulia kundi la wapiganaji wa kiislamu, al-Shabab.

Hali mbaya ya anga na kuwepo kwa wanajeshi kumefanya idadi ya wakimbizi wanaoingia katika kambi ya Dadaab nchini Kenya kutoka Somalia kupungua.
Juma moja kabla ya wanajeshi wa Kenya kuingia Somalia, wakimbizi 3,500 waliingia Kenya.

Juma lililofuata, wakimbizi 100 pekee waliwasili.

"Hali ya usalama bado ni tete, hasa mikoa ya kusini mwa Somalia, na kutatiza shughuli za misaada," Shirika linalotoa misaada kwa raia la Umoja wa Mataifa, Ocha, limesema katika taarifa.

No comments: