Tangazo

October 12, 2011

MWENYEKITI TUGHE NHIF, BARAKA MADUHU ATEULIWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA WADHAMINI TUGHE TAIFA

Mpiganaji Baraka Maduhu (mwenye koti jeusi) ambaye ni Mjumbe wa Kuteuliwa kwenye Baraza la Wadhamini la TUGHE Taifa (National Tughe Board of Trustees) kutoka Tawi la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), akishikana mikono na wenzake kuashiria mshikamano daima "SOLIDARITY FOREVER" katika kusimamia haki wajibu na sheria za kazi kwa watumishi wa Sekta ya Afya na Serikali Kuu,wakati wakitambulishwa kwenye  ofisi za Makao Makuu ya chama hicho  yaliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani. Kulia ni Katibu wa chama hicho, Bw.Kiwenge A.Kiwenge na Mwenyekiti Dkt. Mrutu. Uteuzi huo ulifanywa hivi karibuni na kuhusisha matawi yaliyopo kwenye mikoa sita  nchi nzima na kwa Dar es salaam inawakilishwa na Bw. Maduhu.

Wakipanga mikakati jinsi ya kusimamia majukumu waliokasimiwa kwenye Baraza la Wadhamini la TUGHE Taifa hili kuhakikisha maslahi ya watumishi wa Sekta ya Afya na Serikali Kuu yanakwenda sanjari na mabadiliko ya kiuchumi. Katikati ni Mwenyekiti wa tawi la TUGHE la  NHIF, Bw. Baraka Maduhu ambaye Ameteuliwa rasmi hivi majuzi kuwa mmoja wa wadhamini wa baraza hilo kitaifa. Hongera mpiganaji kwa kupewa nafasi hiyo na uwakilishi mwema.

Wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Makao Makuu ya Ofisi ya Tughe Taifa zilizopo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Bw. J. Mwankenja ambaye ni Mteule Mwenza kitaifa anayemfuatia ni Kamanda Baraka Maduhu Mwenyekiti TUGHE NHIF, Katibu wa Tughe Mkoa wa Pwani, Mzee Kuyunga na mwisho kabisa ni Bi. Fortunat Raymond Mwenyekiti Kamati ya Wanawake TUGHE NHIF. PICHA NA PAUL MARENGA

No comments: