Tangazo

October 20, 2011

MWENYEKITI WA WAMA, MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA UMOJA WA VIKUNDI - MAJOHE

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya  Wanawake na Maendeleo (WAMA),  Mama Salma Kikwete (kushoto) akikabidhi zawadi ya seti moja ya kompyuta kwa  Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi vilivyopo chini ya taasisi hiyo,  Tatu Mwenda (kulia), wakati wa uzinduzi wa  Umoja huo uliofanyika  katika eneo la Nyarugusi, Kata ya Majohe Mkoa wa Dar es Salaam jana Oktoba 19, 2011.  Umoja huo  unajumla ya vikundi 40 vyenye jumla ya watu 700.  Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.
Baadhi ya wanavikundi wakimsikilza Mama Salma Kikwete (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi huo.  
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete (kushoto) akizindua nembo  ya wanakikundi wa  UVIMA wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Umoja huo. Kulia ni Mwenyekiti wa  Umoja huo, Tatu Mwenda.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa  WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia maonyesho ya shughuli  mbalimbali za kazi zinazofanywa na muungano wa wanavikundi vilivyokuwa chini ya Taasisi ya WAMA.  
Mama Salma Kikwete  akitoa hotuba ya uzinduzi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Sadick Mecky Sadick.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya J & L Handicrafts,  Louise Judicate Mushi akionyesha sanaa ya kinyago cha Simba ambacho alikitoa kinadiwe na mapato yatakayopatikana iwe ndio mchango wake kwaajili ya  kusaidia umoja wa vikundi vilivyopo chini ya Taasisi ya WAMA.
Watoto pamoja na kuwa wametoka shuleni na jua ni kali, lakini kwa upendo wao hawakukubali kuenda majumbani mwao na kuamua kushuhudia tukio hilo mwanzo - mwisho.

No comments: