Tangazo

October 24, 2011

RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN AAPISHWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IKULU LEO

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman  kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 24.11. Rais, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia tukio hilo. PICHA ZOTE/JOHN BADI WA Daily Mitikasi Blog
Jaji Mkuu Chande Othman akimkabidhi hati mara baada ya kiapo.
Dk. Shein na Rais Kikwete  wakielekea katika eneo la kupiga picha ya pamoja.
Hapa wakiwa katika picha ya pamoja.
Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja.
Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman  katika picha ya pamoja.
Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Jaji Kiongozi  Fakhi Jundu (kulia), katika picha ya pamoja.
Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Jaji Kiongozi  Fakhi Jundu (kulia), katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Viongozi wengine wa serikali.
Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredreck Werema wakijadiliana jambo mara baada ya hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman wakiburudika kwa vinywaji.
                                            *******************************************
Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dr. Ali Mohammed Shein , ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania  kwa ajili ya kushiriki vikao vya baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni kutokana na Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu 54 ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.

Kiapo hicho kimeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu , Mwanasheria Mkuu, Mawaziri  na maafisa wengine serikalini.

Mara baada ya kula kiapo hicho, Rais Wa Zanzibar amehudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kikiongozwa na Rais Kikwete.

Mara baada ya Baraza la Mawaziri kukamilika jioni leo, Rais anatarajiwa kuelekea Perth Australia kuhudhuria kikao cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kinachofanyika kuanzia tarehe 28-30 mwezi huu.

Kabla ya Mkutano Mkuu kuanza, tarehe 25 October, kutakua  na vikao  kadhaa kikiwemo kikao cha wafanyabiashara ambacho Rais Kikwete anatarajiwa kutoa hotuba ya ufunguzi  na baadae kujumuika na viongozi kadhaa wa  nchi  chache katika kikao maalum na  wafanyabiashara .

Rais anatarajiwa kurejea nchini tarehe 1 Novemba, 2011.

Mapema leo asubuhi Rais amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi kutoka Sudan na Japan.

Balozi Mteule wa Sudan  Yassir Mohamed Ali  amewakilisha hati zake kwanza na kufuatiwa na balozi Masaki Okada.

No comments: