Tangazo

October 24, 2011

Rais wa Zanzibar, Dk. Shein azindua Kikundi cha Taarab cha Tausi Women Musical Club

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akizindua kikundi cha Taarab cha Wanawake cha Tausi Taarab  Wanawake Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli mjini Zanzibar Otoba 22,2011

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akionesha DVD & CD alizozawadiwa na Mbunge na Mlezi wa Kikundi cha Tausi Women Musical Club, Zakia Meghji mara baada ya kukizindua rasmi katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini  Zanzibar Oktoba 22, 2011. Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu Zanzibar
Wasanii wa kikundi cha (Tausi Women Musical Club) wakicharaza ala ya Muziki wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho.
Watoto waliozaliwa katika familia za wanamuziki wa Taarab, Neema Suri (kulia) na Nabil Mohamed wakionesha vipaji vyao katika fani ya kupiga udi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali na wasanii wa kikundi cha Taarab cha Wanawake.

No comments: