Tangazo

October 21, 2011

UN YAENDESHA MJADALA WA HADHARA JIJINI DAR

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akizungumzia msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la Libya wakati alipokuwa akifungua mjadala wa hadhara ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa uliofanyika jana katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya 66 siku ya Umoja wa Mataifa. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou.
Wazungumzaji waalikwa kutoka kushoto Mwendesha Mjadala Bw. Hamza Kasongo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa-TZ Alberic Kacou na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dr. Bohela Lunogelo.
 Baadhi ya wasomi waliohudhuria mjadala wa hadhara ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa uliofanyika leo jijni Dar es Salaam.
Kulia ni Afisa Habari wa UN Information Centre Usia Ledama akiwakilisha wakati wa mjadala huo. Pembeni yake ni baadhi ya wanafunzi wa Vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akifafanua mifumo na mikakati ya Umoja wa Mataifa kwa nchini zinazoendelea wakati wa mjadala huo. Kushoto ni Mhe. Membe.
Nemela Mangula kutoka Centre for Foreign Relation akiuliza swali wakati wa mjadala huo ulionadaliwa na Umoja wa Mataifa ambapo mada iliyokuwa ikijadiliwa ni "Iwapo Tanzania inahitaji Mashirika ya Kimataifa katika siku zijazo".
                                        ********************************

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umeandaa mjadala wa wazi ulioshirikisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu jijini Dar es Salaam huku serikali ya Tanzania ikiwakilishwa na Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe.

Wazungumzaji waalikwa katika mjadala huo uliofanyika jana katika ukumbi wa Karimjee pamoja na Waziri Membe ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa  Alberic Kacou, Mkurugenzi Mtendaji wa wa Economic and Social Research Foundation- ESRF Dakta  H. Bohela Lunogelo huku Msimamizi Muongozaji wa mjadala huo akiwa ni Mzee Hamza kasongo.

Mada kuu uliyokuwa ikijadiliwa katika mjadala huo ni ‘Miaka 50 kuanzia sasa: Mashirika ya Kimataifa yana majukumu katika siku za usoni hapa Tanzania?.

Mjadala huo umeanza kwa Waziri Membe kutoa msimamo wa Tanzania kuhusu vita vinavyoendeleoa nchini Libya huku Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa  Alberic Kacou akifafanua mifumo ya Umoja wa mataifa ikifuatiwa na maswali kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na taasisi .   
Habari na Picha kwa Hisani ya Zainul Mzige wa MO Blog

No comments: