Tangazo

October 21, 2011

WAMA kufanya kazi na GE Health ili kupunguza vifo vya Kinamama Wajawazito na Watoto

Picha ya pamoja baada ya Mwenyekiti  wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete baada ya kumaliza mazungumzo na Ujumbe wa Masuala ya Afya kutoka Marekani  pamoja na Uongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam jana Oktoka 20.2011. PICHA ZOTE/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO
Katibu wa Taasisi ya WAMA, Daudi Nasibu (aliyesimama) akitoa taarifa wakati wa mazungumzo hayo.
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Zakhia Meghji (kulia) akibadilishana mawazo  na wajumbe hao. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi hiyo Janeen Uzzell na  Mkurugenzi Mwenza wa  Mpango wa Ushirikiano wa Wake wa Marais wa Nchi za Afrika,  Cora Neumann.
                                                        ************************************

Na Anna Nkinda – Maelezo

Taasisi ya General Election Health Magination (GE) ya nchini Marekani imeamua kufanya kazi na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ili kuhakikisha kuwa vifo vya wanawake wajawazito na watoto vinapungua hapa nchini.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi hiyo Janeen Uzzell wakati akiongea na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Uzzel alisema kuwa wameamua kufanya kazi na Taasisi ya WAMA kutokana na jitihada zinazofanywa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mama Salma Kikwete  za kuhakikisha kuwa vifo vya kina mama wajawazito na watoto vinapungua kwa kuchangia vifaa tiba katika Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati  na kutoa elimu ya uzazi salama kwa jamii.

“Katika suala la kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto Taasisi yetu inafanya kazi tatu ambazo ni kufuatilia maendeleo ya Mama mjamzito tangu mimba iko changa hadi wakati wa kujifungua, tunatoa  mashine ya kumsaidia mtoto mchanga na mama mjamzito pale ambapo mama atakuwa amejifungua na hana nguvu za kumsaidia mtoto na vifaa tiba vya kuwahudumia wagonjwa wa dharula”, alisema Uzzell.

Kwa upande wake Mama Kikwete aliishukuru taasisi hiyo kwa kuona umuhimu wa kuimarisha afya ya mama na mtoto na hivyo kuamua kufanya kazi  nchini Tanzania kwa ajili ya kukabiliana na  tatizo hilo.

Alisema kuwa Afrika inahitaji kusaidiwa ili iweze kuimarisha afya ya mama na mtoto kwani vifo vya mama na mtoto ni tatizo katika nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania  ili kukabiliana na tatizo hilo Serikali inafanya kila liwezalo ili kuhakikisha kuwa  malengo ya milinia namba  nne na tano yanafanikiwa ifikapo mwaka 2015.

No comments: