Tangazo

November 11, 2011

HALI NI MBAYA HUKO MBEYA -POLISI NA MACHINGA WAENDELEA NA MAPIGANO

Mmoja wa majeruhi wa risasi za polisi katika vurugu za Mwanjelwa leo, Abel Mwalukali akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kupigwa risasi kwenye mkono.
Majeruhi wa risasi za polisi katika vurugu za Mwanjelwa leo hii akiwa kapigwa kichwani. Hadi sasa kuna majeruhi wanne wa risasi, wawili kichwani, mmoja kwenye paja na mwingine mkononi.
Msosi kitu gani bwana mbele ya uhai.

Mabaki ya ganda la risasi.

Mabomu ya machozi pia yalitumika.

Inapotokea patashika nguo kuchanika basi huwa hivi hata mzura huwa mzito kichwani..
Maduka yote eneo la Mwanjelwa mpaka uyole yamefungwa.
Mmachinga akiwarushia jiwe polisi  kwa kutumia manati yaani ni hatari tupu.
Naye mwandishi wetu  wa mbeya yetu Joseph Mwaisango alionja joto ya jiwe baada ya kutupwa ndani ya gari ya polisi kwa kosa la kupiga picha matukio hayo ya wamachinga na polisi  baadaye aliachiwa na kuendelea na kazi yake.
Moja ya gari lililobinuliwa na kuwekwa katikati ya barabara ya Mbeya-Tunduma.
Askari wa kutuliza fujo naye akiwarushia bomu la machozi wamachinga wanaoandamana.
Baadhi ya wamachinga wakiwa wamelipindua gari yaina ya toyota na kusimama juu yake huku wakitamka maneno makali kwa polisi na Jiji la Mbeya kwa kuwanyanyasa katika biashara zao. Kwa ufupi vurugu zinaendelea  zimefika Uyole kati hali si shwali barabara zimefungwa sasa nizaidi ya masaa 10 hakuna usafiri yati Mbeya Iringa wala Mbeya Tunduma habari kamili tutawaketea baadaye.
Moja ya mabango waliyobeba wamachinga hao.Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog

No comments: