Tangazo

November 1, 2011

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA, BLANDINA NYONI AFUNGA KONGAMANO LA WANAHABARI KUHUSU BIMA YA AFYA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni (kushoto) akizungumza na wanahabari baada ya kufunga kongamano la wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu taarifa za tafiti za upatikanaji wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika mjini Morogoro.

Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa akifafanua mambo mbali mbalimbali kuhusu masuala ya dawa na tiba.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni (kushoto) akihutubia alipokuwa akifunga kongamano la wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu taarifa za tafiti za upatikanaji wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika mjini Morogoro.

Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Lauden Mwambona akiongoza mijadala ya tafiti hizo. Kutoka kushoto ni Benny Mwaipaja wa TBC Manyara na Saiboko wa Daily News.

Cosmas Nadimi wa MSD, akijibu maswali mbalimbali ya wanahabari kuhusu usambazaji wa dawa nchini.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika kongamano hilo mjini Moro.

Blandina Nyoni akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Clement Mshana (kulia) pamoja na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Deodatus Balile.

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akitoa majumuisho ya mapendekezo yaliyotolewa na wadau kwenye kongamano hilo.

No comments: