Tangazo

November 14, 2011

MICHUANO YA KIMATAIFA MPIRA WA WAVU YA KOMBE LA NYERERE

Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere
 
Si rahisi kumtenganisha baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na uhuru wa nchi yetu. Kwa kulitambua hilo TAVA inashherekea sherehe za miaka 50 ya uhuru kwa aina yake kwa kumkumbuka Baba wa taifa katika kipindi cha sherehe za miaka 50 ya uhuru. 
 
TAVA inaandaa shindano la kimataifa linajulikana kama "MICHUANO YA KIMATAIFA MPIRA WA WAVU KOMBE LA NYERERE" litakalofanyika mjini moshi katika viwanja vya hindumandal kuanzia tarehe 5 mpak 9 Dec siku ya kilele cha sherehe za uhuru.

Michuano hii inashirikisha vilabu vya wanaume na wanawake kutoka katika nchi jirani za Afrika mashariki. Tunategemea timu kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na pia kutoka Zambia, ambako tayari wamesha patiwa mialiko na kuonyesha nia ya kushiriki. 
 
Timu wenyeji za wanaume na wanawake zitakazo shiriki ni Jeshi stars, Magereza, JKT za Dar, Mzinga ya Morogoro, Polisi Tz, Mafunzo na Nyuki za ZNZ, Kijichi ya Dar, Makongo na lord baden sec schools, Timu za vyuo vikuu vya Moshi KCMC na MUCCoBS, Arusha Volleyball club (AVC), Tanga central na Rukwa Volleyball club.

TAVA inachukua nafasi hii kutafuta wadhamini kujitokeza kudhamini mashindano hayo makubwa kuwahi kufanyika katika historia ya mpira wa wavu nchini kwani ni maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru tukisheherekea na nchi jirani katika michezo.

Kwa mawasiliano zaidi:-
 Alfred Selengia,
M/kiti - kamati ya maendeleo ya mpira wa wavu - TAVA
0655 710302

Katibu Mkuu wa TAVA
Allen Alex
0713 550798

No comments: