Tangazo

January 25, 2012

WAZIRI MAGUFULI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KIVUKO CHA MSANGA MKUU

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (Kulia) akipata  taarifa ya  maendeleo ya ujenzi wa kivuko cha Msanga Mkuu  kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Marcellin Magesa (kushoto)  katika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba watu 100 pamoja na kubeba tani 50 za mizigo kimegharimu shilingi 2,8 bilioni za serikali ya Tanzania, Kupatikana kwa kivuko hicho ni kati ya utekelezaji wa ahadi aliyotoa Rais Jakaya  Kikwete kwa  wakazi wa Mtwara vijijini,  watakaofaidika na kivuko hicho, pamoja na vijiji vitano vya  Namera, Sinde, Mkubiru, Mnete pamoja na Msanga Mkuu yenyewe vyote vipo Mtwara vijijni  . (Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

Sehemu ya kivuko kwa nyuma.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kushoto) akipata maelezo ya ramani kuhusu ujenzi wa kivuko cha Msanga Mkuu leo  kutoka kwa Meneja mradi Peter van  Bruggen (mzungu).



Mafundi wakiwa kazini wakiendelea na ujenzi wa kivuko.


Waziri Magufuli akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho.

Waziri wa Ujenzi DKT. John Magufuli (alievaa kofia) akifuatiwa  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambae vilevilie ni Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia (mwenye mtandio) wakiteremka kwenye kivuko cha Msanga Mkuu.

No comments: