Tangazo

February 7, 2012

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) WAKAGUA VITAMBULISHO KWA WANACHAMA WAKE

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bw. Immanuel Humba akifafanua mbele ya wanahabari  kuhusu zoezi la ukaguzi wa vitambulisho kwa wanachama wake kwenye hospitali na vituo mbalimbali vya kutolea huduma,kumekuwepo kwa matumizi yasiyo sahihi kwa wanachama wachache wasio waaminifu, amewataadharisha wanachama watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mkurugenzi wa Operesheni, Bw. Eugin Mikongoti akiwaeleza waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa zoezi la ukaguzi wa vitambulisho vya wanachama wa NHIF, ambapo amewataka wanachama,waajiri na watoa huduma kulipokea kwa mtazamo chanya na kutoa ushirikiano kwani una lengo la kudhibiti wanachama wasio waaminifu ambao wana lengo la kudhoofisha malengo ya mfuko huo. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Immanuel Humba na (wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji, Bw. Deusdedit Rutazaa.

No comments: