Tangazo

March 7, 2012

BONDIA SELEMANI GALILE KUGOMBANIA UBINGWA WA TPBO DHIDI YA THOMAS MASHALI

MKANDA wa ubingwa wa ngumi za kulipwa wa TPBO (Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa) unatarajia kuwaniwa April 9 mwaka huu Dar es Salaam.

Mkanda huo ambao upo wazi utawaniwa na bondia kati ya Thomas Mashali na Selemani Galile uzito wa kg 75 middle weight.

Akizungumza Dar es Salaam na blogu hii, juu ya maandalizi yake, Galile alisema amejiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua mkanda huo ambao upo wazi kwa sasa.

"Naendelea kufanya mazoezi yangu kwa ajili ya kuwania mkanda huu ambao ninaamini utaweza kunitambulisha ubora wangu katika tasnia hii ya masumbwi,"alisema Galile.

Alisema kuhusu mpinzani wake Mashali hana hofu naye kwa kuwa mchezo huo huamua nani mkali atakayetwaa ubingwa wakati wakiwa ulingoni na si nje ya hapo na kwa sasa nimepata staili mpya za mabondia wa dunia.

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa Kimataifa wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye,Lenox Lewis,Evalnder Holfilder na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

No comments: