Tangazo

April 19, 2012

Airtel yatoa Kompyuta na Vitabu vya Milioni 25/- kwa Chuo Kikuu cha Dodoma

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi baadhi ya vitabu  vya chuo kikuu vilizotolewa na Airtel kwa chuo kukuu cha Dodoma (UDOM) kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula (kulia) jana wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika chuoni hapo.  anaeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Bi Betty Mkwasa (kati). Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote vyenye  thamani ya Milioni 25/-  ikiwa ni muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.

Mkuu wa wilaya ya Bahi, Bi Betty Mkwasa akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana pamoja na wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya wanafunzi wa IT chuoni hapo wakiwa wameshikilia vitabu vilivyotolewa msaada na Airtel kwa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS  toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini.
*****************

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote vyenye thamani ya milioni 25/- TZS kwa chuo kikuu cha Dodoma ikiwa ni muendelezo wa shughuli zake za kijamii  katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.

Kompyuta hizo pamoja na vitabu  vimekabidhiwa  kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kilichopo mkoani Dodoma jana wakati wa hafla fupi iliyofanyika ukumbi mdogo wa mikutano chuoni hapo na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Bhahi Mh, Betty Mkwasa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya wa Bhahi aliishukuru Airtel Tanzania kutokana na jitihada zake za kushirikiana na serikali katika kusaidia sekta mbali mbalimbali ikiwemo elimu.

No comments: