Tangazo

June 4, 2012

Mamia ya wananchi wamejitokeza kwa wingi kwenye mbio za Susan G.Komen za Mapambano dhidi ya Maradhi ya Saratani ya Matiti 2012

Wananchi hao wakiwemo waTanzania walikusanyika katika viwanja vya Down Town Washington DC siku ya Jumamosi June 2.2012 katika kuitikia wito wa kuunga mkono wanawake ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa saratani ya matiti, utafiti na elimu dhidi ya ugonjwa huo. (Picha maelezo na swahilivilla.blogspot.com)

Kina dada wa Kitanzania wakiwa katika matembezi ya kupiga vita Ugonjwa wa saratani ya matiti siku ya Jumamosi June 2.2012 ndani ya Washington D.C nchini Marekani.

Rais wa Jumuia ya wa Tanzania DMV (Kutoka Kushoto), Mh. Iddi Sandaly, Waheeda Margaret Gathesha, Chief wa swahilivilla Abou Shatry, Aunt Rehema, pamoja na Salma Jay Jay pia alikuwepo katika matembezi hayo.

Wazawa wa kitanzania wanaoishi nchini Marekani wakiwa katika matembezi ya kupiga vita ugonjwa wa saratani ya matiti.


Team Tanzania waki wakiwa kipata picha ya pamoja  katika kuitikia wito wa kuunga mkono wanawake ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa saratani ya matita, utafiti na elimu dhidi ya ugonjwa huo.

No comments: