Tangazo

July 18, 2012

African Barrick Gold (ABG) yatoa Msaada wa Chakula Shinyanga na Geita

Kutoka Kushoto: Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya wakipokea msaada wa sehemu ya tani 200 za mahindi kutoka kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof (wa pili kulia)na Makamu wa Rais wa African Barrick Gold (ABG),Utekelezaji Muundo, Peter Gereta katika hafla iliyofanyika katika Kata ya bulyanhulu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga hivi karibuni. Maeneo yatakayonufaika na msaada huo uliogharimu kiasi cha milioni 163/- ni kwa wale waliokumbwa na uhaba wa chakula katika vijiji 14 vilivyoko Bugarama, Mwingiro na Bulyanhulu wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga na Nyang'hwale Mkoa  mpya wa Geita. Picha zote/John Badi wa Daily Mitikasi Blog

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya akipokea msaada wa tani 200 za mahindi kutoka kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof (wa pili kulia). Kushoto ni Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, Joseph Makoba.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya akihutubia kabla ya makabidhiano. Kulia ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof  na Kushoto ni Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, Joseph Makoba na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa akihutubia kabla ya makabidhiano.

Sehemu ya viongozi wa vijiji lengwa na msaada huo  waliohudhuria hafla hiyo.

Kutoka Kushoto: Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof , Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa wakikagua sehemu ya shehena ya mahindi mara baada ya makabidhiano.  

Viongozi wa African Barrick Gold wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya makabidhiano.

Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof (katikati), na Makamu wa Rais wa African Barrick Gold (ABG),Utekelezaji Muundo, Peter Gereta.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Dennis Hoof akijadiliana jambo na  Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya.

No comments: