Tangazo

July 19, 2012

Madiwani Kigoma Vijijini watakiwa kuwa na Upeo wa Katiba ya Zamani wakati wakijiandaa na Mchakato wa Katiba Mpya


Na Magreth Magosso, Daily Mitikasi Blog - Kigoma

Halmashauri ya wilaya ya Kigoma Vijijini imekabidhi Katiba 18 kwa Madiwani wake ili kuwapa upeo wa mchakato wa uundwaji wa katiba mpya .

Hayo yamedhihirika juzi mkoani hapo kwenye Kikao cha Madiwani kipindi cha robo ya nne 2011-2012, ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Miriam Mbaga alisema kwamba, lengo la kuwapatia katiba hizo ni kutoa elimu ya katiba ya sasa kwa wananchi wao ili wapate fursa ya kutoa mawazo ya mchakato mzima wa katiba mpya.

Mbaga alisema kwamba,kutokana na changamoto ya  kata  za kusini kuwa na miundombinu duni  hasa ya kusini, imemlazimu kuwapatia katiba 12 ili wanakijiji wapate fursa ya kujadili na kung’amua mapungufu ya katiba ya sasa ikiwa na tija ya katiba ijayo.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa,kutokana na mazingira ya mkoa huo, amewapatia  motisha ya vitenge 60 madiwani 31 wa halmashauri hiyo ili kuwahamasisha watende kazi kwa bidii ili kuondoa mkoa huo katika wimbi la umaskini kwa wapiga kura wao.

Mbaga alisema kwamba,kutoa motisha ya vitenge hivyo ni sehemu yake kwa wadau wake wakiwemo madiwani ili kuwajengea ujasiri wa kuwa karibu hali itakayochochea kufunguka kwake na kubaini changamoto zilizoko

No comments: