CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA) kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa chama
hicho utakaofanyika Desemba 21 na 22 mwaka huu Kiromo View Resort Hotel, Bagamoyo mkoani
Pwani.
Kama
tulivyosema wiki iliyopita kuwa mkutano huo unatarajiwa kushirikisha wanachama zaidi
ya 100, ambao kushiriki kwao itabidi wathibitishe kwa njia ya maandishi kwa
maana ya email ili uwepo wao uweze kuthaminika.
Lakini
bado kuna mwitikio mdogo wa wanachama wanaothibitisha ushiriki wao, ambapo hadi
kufikia leo saa tano asubuhi waliothibitisha ni 22 tu, hivyo tunasisitiza
wengine wafanye hivyo haraka na tusikubali kufanya mambo kwa mazoea na mwisho
wa kuthibitisha ni Jumamosi Desemba 15, saa kumi alasiri na watakaokwama
kufanya hivyo watahesabika wamekosa sifa ya kushiriki mkutano.
Tunaomba
wanachama wote ambao wanatarajia kuhudhuria mkutano huo wathibitishe ushiriki
wao kwa Katibu Mkuu wa TASWA kwa njia ya email: mgosius@yahoo.com au taswatz@yahoo.com.
Kamati
ya Utendaji ya TASWA inaendelea na juhudi za kutafuta wadhamini kwa ajili ya
Mkutano Mkuu, ambapo kiasi cha Sh. Milioni 20 kinahitajika kufanikisha mkutano ikiwa
ni gharama mbalimbali ikiwemo chakula, malazi, usafiri kwa wanachama wa Dar es
Salaam, pamoja na usafiri na malazi kwa wanachama wanaotoka nje ya Dar es
Salaam.
Tayari
wadau watatu wamejitokeza kupiga jeki mkutano huo, ambapo Alhamisi Desemba 13
saa tano asubuhi mgahawa wa City Sports Lounge Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto
atatangaza mdhamini mmoja ambaye tutakuwa tumemalizana naye.
Kiasi
cha fedha kinachohitajika ni kikubwa sana, hivyo bado jitihada zinaendelea
kutafuta wadhamini wengine kuhakikisha mkutano unakuwa wa mafanikio makubwa na
tunaomba wenye nia ya kushirikiana nasi wafanye
hivyo.
Licha
ya wanachama pia tunatarajia katika mkutano huo pia watakuwepo wadau mbalimbali
wa TASWA wakiwemo waandishi wakongwe wa habari za michezo ambao watapewa nafasi
ya kuzungumza.
Wanachama
wa TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili Ripoti ya Utendaji ya chama,
Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na masuala mbalimbali yanayohusu waandishi
wa habari za michezo kwa ujumla.
Pia
kutakuwa na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo ili wawe
na uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo itajadiliwa
kwenye mkutano huo.
Kamati
ya Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea
kwa kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza iwaite
wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo hilo na kukishakuwa na
uelewa wa kutosha suala hilo lipelekwe kama ajenda kamili ya kuanzisha chama
hicho kwenye Mkutano Mkuu.
Imetolewa na:
Amir
Mhando
Katibu
Mkuu TASWA
10/12/2012
No comments:
Post a Comment