Na Mwanakombo Jumaa- Maelezo, Arusha
Vijana nchini wameshauriwa kuzitumia vizuri fedha za mkopo wa mfuko wa maendeleo ya vijana ili kuwawezesha kukuza uchumi wao na hivyo kuondokana na umaskini.
Hatua hii pia itawawesha kukuza kipato chao na hivyo kubadilisha maisha yao hatua ambayo itasaidia kupunguza tatizo la ajiira nchini kwa makundi ya vijana.
Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara wakati wa ziara yake ya kuvitembelea vyama vya ushirika wa akiba na mikopo (Saccos) mbalimbali viliv yopata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana unaosimamiwa na wizara hiyo.
Mfuko huo ambao lengo lake ni kuwasaidia vijana ama vikundi vya vijana ili waweze kujiajiri kupoitia shughuli za uzalishaji mali na miradi ya kiuchumi.
Dk. Mukangara amesema mikopo inayotolewa na wizara yake ni jitihada za serikali kuwasaidia vijana na wajasiliamali ili waweze kujikwamua kiuchumi katika maisha, hivyo alisisitiza suala la uaminifu, nidhamu na uadilifu katika kutumia mikopo hiyo likiwemo suala la vijana hao kurejesha kwa wakati mikopo hiyo.
Akiwa katika kutembelea saccos ya soko kuu waziri Dk. Mukangara alielkezwa na katibu wa ushirika huo Philipo Kullaya kuwa ushirika huo una wanachama wapatao 597 ambapo asilimia 70 ni vijana.

Alisema ushirika huo umefanikiw akuwapatia wanachama wake wakiwemo vijana mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 847.
Aidha alimweleza waziri kuwa saccos hiyo kwa mwaka 2009/2010 ilifanikiw akupata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wamaendeleo ya vijana unaosimamiwa na wizara yake ambapo vijana wapatao 22 walinufaika na fedha hizo.
Kufuatia hali hiyo Waziri Dkt. Mukangara amefarijika kuona wajasirirmali ni kwa jinsi gani wamenufaika na fedha hizo na jinsi walivyoweza kurejesha mikopo kwa wakati.
Amesema hatua hii imesaidia kuwawezesha vijana kuwatengenezea ajira za uhakika na pia kutengeneza ajira kwa vijana wengine mkoani Arusha.
Hata hivyo wanaushirika hao walimweleza waziri huyo kuwa wanakabiliw ana changamoto kubwa ya kukosa elimu ya ujasiriamali pamoja na mitaji midogo ili kupanua wigo kwa vijana wengi kuweza kupata mikopo kutoka mfuko huo wa maendeleo ya vijana.
Katika ziara yake pia ameziagiza taasisi za wizara yake ikiwemo Idara ya Habari (MAELEZO) , Kampuni ya magazezi ya Serikali (TSN) na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) zifanye kazi kwa kushirikiana
Waziri Mukangara amesisitiza kuwa hivi ni vyombo vya serikali na hivyo vinapaswa kutetea sera za serikali pamoja na kujibu hoja mbalimbali zinazozoikabili serikali kwani vyombo hivi ndio mdomo wa Serikali.
Katika ziara yake amevitembelea ushirika wa PETU SACCOS, Soko KUU SACCOS pamoja na Krokon SACCOS ambapo alipata fursa ya kuongea na viongozi pamoja na wanachama.
No comments:
Post a Comment