Tangazo

February 21, 2013

WADAU WAZIDI KUJITOKEZA KUMSAIDIA MTOTO OMBENI

Mtoto Ombeni akiwa amelazawa katika Hospitalini ya General mjini Dodoma akipata matibabu baada ya kupata ajali ya moto Desemba 14 2012. Pichani mmiliki wa blog ya Pamojapure akimfariji mtoto Ombeni baada ya kumtembelea hospitalini alikolazwa.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wakati hali ya mtoto Ombeni Mbeula ambaye amelazwa katika Hospitali ya General iliyopo mjini Dodoma ikiwa bado si nzuri baadhi ya wadau wameanza kujitokeza kwa ajili ya kumpa msaada wa kupata matibabu.

Mtoto Ombeni ambaye alipata ajali ya moto huko Mpwapwa alifikishwa hospitalini hapo tarehe 14/12/2012 kwa sasa mtoto huyo ameanza kupata matibabu baada ya habari zake kurushwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo kwa sasa madaktari wa hospitali ya General wameanza kumpatia matibabu mtoto huyo baada ya kukosa huduma hiyo kwa kipindi cha miezi miwili kutokana na wazazi wake kukosa fedha za matibabu. 

Kwa moyo wa dhati tunawashukuru wale wote waliotoa michango yao kupitia kwenye namba ya ndugu yake ambayo ni Ekiria Paskali na namba yake ya simu ni 0757 498336 Hawa ni baadhi ya wale walioguswa na tukio hilo na kutoa mchango wao wa hali na mali.

Kwa mujibu wa habari kutoka kwa mmiliki wa Blog Pamojapure michango iliyopatikana kutoka kwa wadu ni jumla ya shilingi 421,300 ambazo zitamsaidia mtoto huyo katika matibabu yake na wadau wameombwa kujitokeza ili kunusuru maisha ya mtoto huyu. Kama umeguswa na matatizo ya mtoto huyu unaweza kumchangia mtoto huyu apate matibabu tuma mchango wako kwa kutumia namba hii 0757 498336 mwenye jina lake ni Ekiria Paskali

No comments: